tanga kwetu
JF-Expert Member
- May 12, 2010
- 2,193
- 1,441
Kwa muda mrefu sasa, maharamia (Pirates) wa kisomali wamekuwa wakitesa kwenye mwambao wa bahari ya hindi ndani ya himaya ya Tanzania kama vile wahusika wapo likizo. sasa imefikia wanafika hadi ndani ya kilometa 220 toka ufukweni na kuwa-harass wavuvi wadogo wadogo huko Lindi na Mtwara. Mbaya zaidi Chief of staff (Alhaji sheikh Ustaadh Lt. Jenerali Shimbo) anataka kulipa jeshi jukumu la kupiga raia watakaotaka kuipigania haki yao ambayo imeshaandaliwa mazingira ya kuchakachuliwa. Kuna usemi fulani wa kitoto 'kama una nguvu, pigana na ukuta' nami nasema 'kama mna nguvu, furumusha hao Somali Pirates'