Ndugu Zitto, Ben, Mamuya, Kitilya na 'Maslia',
Napenda kuwakumbusha kwamba Mwl J. K. Nyerere aliendesha harakati za kuikomboa nchi yetu akiwa kijana. Ninasikitika sana, tena sana kusikia mipango na mikakati kabambe ya kutaka kukwamisha harakati za ukomozi wa pili wa nchi yetu, UKOMBOZI AMBAO HAUPUKIKI! Nasema hauepukiki kwa sababu ya hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa leo, mtanzania ambaye hana uhakika wa mlo wa siku, mtanzania ambaye hana maji ya uhakika, mtanzania ambaye hana uhakika wa kusoma, mtanzania ambaye hana uhakika wa matibabu (hili linaniuma zaidi kwani kwenye hospitali kubwa kama Muhimbili hupati huduma mpaka uzungumze vizuri!), mtanzania ambaye hana uhakika wa kusafiri kwa njia rahisi (gari moshi) achilia mbali kusafirisha mizigo, mtanzania ambaye hana umeme achilia mbali mgawo wa umeme.
Mimi kama kijana msomi (sijisifii) nilidhani vijana tumebeba matumaini ya watanzania walio wengi (maskini) na tunapigana kwenda mbele kuleta mwanga lakini kumbe ni kinyume chake. Mimi ni mojawapo ya watu ambao walikuwa nyuma ya Zitto nikiamini kuwa ni mpiganaji wa kweli, lakini hivi karibuni nimepoteza matumaini na huyu kijana mwenzangu kwa sababu ya hatua na misimamo yake mbalimbali ambayo amekuwa akionesha waziwazi ambayo kwa maoni yangu si matarajio yangu kwa mwanamapinduzi. Malumbano haya yamenisaidia kukubaliana na wasiwasi wangu juu ya Zitto. Naamini Zitto atanielewa kuwa simhukumu ila historia ndio itakayomhukumu.
Mwisho, nakishauri chama cha CHADEMA kuchukua hatua madhubuti na za busara kusaidia kunusuru chama hiki kilichobebe matumaini mapya kwa Watanzania. Ninawatia moyo wote wenye mapenzi mema na nia njema ya kupigania haki, usawa na ustawi wa Mtanzania popote alipo, Mungu yupo upande wetu! Huu ni mwanzo tu, wasaliti wote wataumbuka na watajitaja wenyewe kama hawa walivyofanya.
Kamwe tusikubali kurudi nyuma kwa sababu ya wanaharakati uchwara hawa wanaohangaika kila kukicha ili kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa Tanzania yetu. kumbukeni, bado tuna safari ndefu na daraja refu la kuvuka ili kuikomboa nchi kwa mara ya pili baada ya miaka hamsini ya UKIRITIMBA, UZANDIKI, na UFISADI
Mungu ibariki CHADEMA
Mungu ibariki TANZANIA
Mungu waumbue WANAFIKI
AMEN.