dengue f
Member
- Jun 4, 2017
- 18
- 47
Kufuatia tukio la kujiua kwa kijana Musa Ally aliyejirusha kutoka juu ya Jengo la Rock City Mall huko Mwanza, nitoe rai fupi.
Musa ameacha ujumbe unaoashiria kuwa sababu ya kujiua kwake ni kukosa ajira. Lakini kukosa ajira hakuwezi kuwa sababu ya kujiua, bali ni sababu iliyopelekea Musa kupata maradhi ya akili, kisha kujiua.
Mara nyingi kujiua, au kufikiria kujiua ni matokeo ya maradhi ya akili, kwa kesi ya Musa tunaweza sema ni maradhi ya Sonona (Depression), au "Bipolar Mania" au mengineyo. Baada ya kipindi cha sononeko, kujitahidi na hatimaye kukata tamaa, mtu hukosa sababu ya kuendelea kuishi. Mipango yake na matarajio yake vimeyeyukia hewani. Mwanga wa jua unamfanya kipofu, usiku wa giza unamuumiza macho, hakuna kinachomsaidia, au kwa ufasaha zaidi, hakuna anachoweza kukifanya kimsaidie, kwa sababu ni mgonjwa. Kwahiyo huamua kujiua.
Kujiua hutokea baada ya kufikiria mara kadhaa kufanya hivyo, au wakati mwingine mtu hujaribu kujiua bila kufanikiwa. Akirudia jaribio lake la kujiua, hufanya kwa uhakika ili asishindwe tena. Jambo la uhakika ni kuwa, kama Musa alikuwa na Sonona, basi alikwisha kuwaza kujiua kabla ya siku ya kifo chake. Kujirusha kutoka juu ya jengo refu, ni tendo la uhakika wa kujiua.
Uwepo wake juu ya jengo refu unaweza kuwa kichocheo, pengine angekuwa chini asingekufa. Pombe inayosemekana kwamba alikunywa, pia inaweza kuwa kichocheo. Pombe inasababisha athari ya kisaikolojia inayoitwa 'Disinhibition effect', ambapo mtu hushindwa kujizuia na matendo ya hatari anayowaza kuyafanya akiwa amelewa.
Zaidi kuhusu Sonona tunaweza kuelezana baadaye, leo hoja zangu ni mbili.
Kwanza, ni vema jamii ikaanza kuyapa kipaumbele maradhi ya akili, ambayo yapo kwa watanzania wengi. Na athari zake zinaonekana kwenye jamii yetu. Bahati mbaya tunayachukulia maradhi ya akili tofauti sana. Badala ya kwasaidia wagonjwa tunawapa majina ya dhihaka, kama vichaa, mataahira, mtambo, network error', dishi limecheza nk. Pengine watu hawa wangeweza kusaidiwa na kupona, lakini tunapuuza. Baadaye unasikia mtu amejiu, au ameua mke au mume au mtoto na kumkatakata kama nyama ya buchani, ni maradhi ya akili.
Pili, pasina lengo la kumtupia lawama mtu, lakini nathubutu kusema wizara inayohusika na vijana na ajira, imeshindwa kuwasaidia vijana. Tanzania 'imejifungia' chumbani wakati huu wa ulimwengu wa teknolojia na mawasiliano. Kuna fursa nyingi za ajira kwa vijana endapo tutawapa vijana nafasi ya kujipambanua kimataifa. Zipo kazi nyingi za kuingia kipato kupitia mitandao, lakini kwa mifumo ya kifedha ya Tanzania, haziwezekani. Kuna michezo mingi duniani, karibu kila siku kuna mashindano makubwa ya michezo ya kimataifa sehemu fulani duniani, watanzania wamejifungia chumbani.
Yapo mambo mengi mepesi, ambayo vijana wa nchi zingine wanafanya, lakini huwezi kufanya ndani ya Tz kwa sababu za kimfumo.
Tunahitaji mabadiliko makubwa, kwenye mifumo yetu ya elimu, shuleni, vyuoni na mitaani.
Musa, ni mtu mmoja ambaye amefikia kujiua, wapo waliokwisha kujiua na watakaojiua. Lakini athari za Sonona sio kujiua tu, ni pamoja na kuua wengine au kufa bila kujiua. Wengine wanaweza wakabaki hai, lakini wakashindwa kufanya chochote maishani hadi wanakufa.
Let's get up. Tuzungumze kujisaidia na kuwasaidia wengine.