Justice for Mchome

Justice for Mchome

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
828
Reaction score
2,109
Kuna mambo yanastaajabisha na kutia hasira sana. Wiki iliyopita Mwenyekiti wa BAVICHA mkoani Kilimanjaro, Lembruce Mchome alikamatwa mkoani Arusha kwa tuhuma za kupiga picha gari ya Mkurugenzi mkuu wa Usalama wa Taifa Kamishna Diwani Athumani Msuya alipokwenda nyumbani kwao Mwanga.

Hayo ndiyo mashtaka aliyofunguliwa kituo kikuu cha polisi Arusha. Lakini baadae alisafirishwa kuja Dar na hakupelekwa mahakamani kwa zaidi ya wiki moja. Leo amepandishwa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka ya kusambaza picha za ngono mtandaoni. Yani "charge sheet" imebadilika kutoka kupiga picha gari ya DG wa TISS hadi kupiga picha za ngono.

Unaweza kujiuliza hiyo gari ilikua na maudhui ya ngono au camera aliyotumia ilibadilisha picha za gari kuwa za ngono? Funny but not funny. Au unaweza kuwaza pengine kwa wiki moja polisi waliyokaa nae wamejiridhisha kuwa wangemfungulia kesi ya kupiga picha gari ya usalama wa taifa angewashinda. Pengine si jinai kupiga picah gari ya boss wa TISS. Mbona ya IGP inapigwa picha tukikutana mtaani na haijawahi kuwa big deal.

Lakini kama kweli alipiga picha za ngono na ushahidi wanao kwanini hawakumpeleka mahakamani walipomkamata kule Arusha? Kwa nini wakae nae zaidi ya wiki moja mahabusu? Walikua wanajadili nini wakati sheria inasema ndani ya saa 24 mtuhumiwa apelekwe mahakamani?

Na kwanini kosa lifanyikie Mwanga (Kilimanjaro), mtuhumiwa akamatiwe Arusha halafu apandishwe mahakamani Kisutu? Kwanini hakupelekwa Mwanga anakodaiwa kutendea kosa hilo akashtakiwe huko?

Halafu amenyimwa dhamana wakati kosa hilo linadhaminika. Hakimu anasema amemnyima dhamana baada ya mawakili wa serikali kudai kuwa mshtakiwa akiwa nje ataharibu ushahidi. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 2 Juni 2020 na Mchome amepelekwa rumande gereza la Segerea.

#Justice4Mchome
......
Malisa GJ

Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
Mku kwa sasa kuna tatizo kubwa sna cdm.hawa vijana ni wazuri sna ila hakuna wakuwaongoza na kuwatetea pale wanapopata shida.cdm si kama ile ya miaka ya slaa ndo maana viongzi waandamizi wanawafanyia watakalo uku ata mawakili wao wamewachoka maana kesi ni nyngi.ni wakati sasa chama kuingia darasani kusoma mchezo nakubadili fomula.fomula hi imepitwa na wakati.
 
Unamasihara upige picha upeleke wapi? Ya nini?

1. Je ulitaka kuteka gari
2. Ulitaka kuliiba unalitafutia soko
3. Unataka kumdhuru mwenye nalo
4. Unataka kumuuwa dereva
5. Unataka kumuuwa mkurugenzi wa TISS
6. Umetumwa na magaidi uwape picha
7. Umetumwa na chama chako umuuwe
8. Umetumwa na adui zake wamuuwe

9. Upo Kenney kundi la ugaidi au genge la kuteka watu.

10. Umetumwa na nani hasa

Huyu dogo namwonea hutuma maana kesi hii itamchukua muda sana kuipambania

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Unamasihara upige picha upeleke wapi? Ya nini?

1.je ulitaka kuteka gari
2.ulitaka kuliiba unalitafutia soko
3.unataka kumdhuru mwenye nalo
4.unataka kumuuwa dereva
5unataka kumuuwa mkurugenzi wa TISS
6umetumwa na magaidi uwape picha
7.umetumwa na chama chako umuuwe
8.umetumwa na adui zake wamuuwe

9.upo Kenney kundi la ugaidi au genge la kuteka watu.

10.umetumwa na nani hasa

Huyu dogo namwonea hutuma maana kesi hii itamchukua muda sana kuipambania

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Acha atie akili kwanza
 
Mawakili wakamtetee atashinda.

Inji hii mida mingine haisomeki someki tu
 
Huyu mpuuzi alisaidiwa akanusurika kwenye utawala wa giza na wa majambazi sasa kaungana na majambazi !
 
Unamasihara upige picha upeleke wapi? Ya nini?

1. Je ulitaka kuteka gari
2. Ulitaka kuliiba unalitafutia soko
3. Unataka kumdhuru mwenye nalo
4. Unataka kumuuwa dereva
5. Unataka kumuuwa mkurugenzi wa TISS
6. Umetumwa na magaidi uwape picha
7. Umetumwa na chama chako umuuwe
8. Umetumwa na adui zake wamuuwe

9. Upo Kenney kundi la ugaidi au genge la kuteka watu.

10. Umetumwa na nani hasa

Huyu dogo namwonea hutuma maana kesi hii itamchukua muda sana kuipambania

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
lakini mashataka yaliyofunguliwa tofauti kbs na ulichotaja wewe!!!!!!
 
Back
Top Bottom