justice delayed is justice denied | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

justice delayed is justice denied

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kinepi_nepi, Nov 26, 2008.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hatimaye watuhumiawa wa The LIST OF SHAME by. Dr. Wilbroad Slaa waanza kuonekana mahakamani.
  Mpiganaji Slaa nakupa hongera nimerejea list ile na tuhuma alizo nazo MRAMBA na Yona ndizo hizo hizo ambazo JK amewafikisha nazo mahakamani. Ni lazima JK akupe hongera na akushukuru.
  Watanzania wote tupo nyuma yako.

  Kikwete anakwenda mwendo wa kinyonga kutimiza wajibu wake anakuwa kama hataki hana uwezo wa kufanya maamuzi ya kiraisi na kiutendaji, haitaji sifa yeyote huu ni wajibu wa utawala wa sheria na unaofuta katiba.

  katiba ya tanzania ipo wazi , Binadamu wote ni sawa mbele yasheria ila JK anatuonyesha watanzania sio sawa mbele ya sheria.

  Ikumbukwe South Afrika walipigania usawa mbele ya sheria na wengi walikufa kwa mapigano hayo mpaka sheria ikaleta usawa kwa wote.

  Marekani vivyo hivyo weusi walibaguliwa kwa kukiuka katiba wengi waliuwawa na wengi waliteswa , waliamua kupigania uswa ulioandikwa kwenye katiba kwa kumwaga damu, rejea Dr. martin luther king na wengine wengi.

  Tanzania hatuwezi kupata usawa na haki ya katiba yetu bila kuipigania.
  Iweje leo tuone ni ajabu Yona kushitakiwa?
  Iweje leo tuone ajabu Mramba kushitakiwa??
  Iweje leo iwengumu kwa Rostam Azizi kushitakiwa????
  Iweje leo Manji kuogapwa na walinda sheria ???
  Iweje leo Rais wa nchi kutaka pongezi kwa kuachia wezi na wahujumu wa mali ya umma kufikishwa kwenye mikono ya sheria???

  hapa kuna tatizo kubwa.
  Viongozi hawajui wajibu wao, wakitimiza wajibu wao inaonekana ni 'favor' kwa wananchi. 'i am sick of this'
  Kikwete ikumbukwe wote ni sawa mbele ya sheria na kuchelewesha haki ni kuikataa haki.
  kikwete huhitaji high pressure ndio utende ni wajibu wako kufanya kazi tuliyokutuma na kufuata sheria.

  Ni vyema akarejea List of shame aangalie ni nani amebaki aburuzwe mbele ya sheria.
  Na wizi wote ambao haujaguswa wezi wote wakajibu mbele ya sheria kama wale wa : Meremeta, Tango gold, Richmond, twin tawer, radar, bandari, nk

  Slaa; wakati umefika kuongeza pressure kwa yote mliyoanzisha, tukumbuke tunadili na utawala uliozimia na unaendeshwa na mashine za uhai hivyo tukipunguza nguvu nao unakwenda likizo. Hii si kwa manuifaa ya kisiasa tu bali kwa ajili ya kizazi kijacho.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,577
  Likes Received: 18,555
  Trophy Points: 280
  Yes its very true indeed that 'Justice Delayed is Justice Denied' but 'Justice must not only be done, but must be seen to be done'. In such a situation better be late than sorry. Serikali iliamua kuchelewa ili iwe na uhakika.

  Naomba usishangilie sana kesi kufikishwa mahakamani, mara ngapi serikali imeshindwa?. Tuiachie haki ufuate mkondo wake.
   
 3. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna kushangilia, ila ni lazima tujue mahakamani ni nisehemu pekee ya kutoa haki. Hawa mbwana wametuhumiwa siku nyingi sana kwa makosa mbalimali ya rushwa , wizi na matumizi mabaya ya nyadhifa zao na walikuwa wawaona watanzania ni malimbukeni.

  Pamoja na kwamba inawezakuwa tunapigwa kiini macho lakini wapo mbele ya sheria sasa ni kazi ya DPP na hao wanasheria wa serikali tuone ni wataalamu au vihiyo. Kwa kesi hii wanaweza kuibua vyote , kiwira , nbc nk.
  Kila mwananchi anatakiwa kujua anaweza kulala keko kwa makosa yake sio baadhi ya watu tu. For this, i like it. Kwa wao kulala keko ni hatua na kwa wao kwenda jela kazi ipo. Rejea Nalaila kiula tulilishwa kasa.
   
 4. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2008
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kaka, maneno yako ni mazito sanaaa!!!!!!!!!

  Inatia uchungu lakini inafurahisha, tupo pamoja brother.

  cheers.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa hakuna kushangilia wala kuchekelea historia inaonyesha Mawaziri wote walio wahi kushitakiwa walishinda kesi zao,

  1 ) Fundikira alifikishwa mahakamani baada ya kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa miaka michache tangu Tanganyika ipate uhuru. Hata hivyo, alishinda kesi.

  2 ) Venance Ngulla, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya pili katika miaka ya 1990. Ngulla alikamatwa na kufikishwa mahakamani katika miaka ya 1990,naye alishinda kesi.

  3 ) aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Nalaila Kiula, katika serikali iliyokuwa chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika miaka ya 1990. Kiula alikamatwa na kufikishwa mahakamani chini ya uongozi wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, kwa tuhuma za rushwa. Hata hivyo, naye pia alishinda kesi.

  4 ) Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya pili, Augustine Mrema naye alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatuhumu hadharani baadhi ya viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali kwamba, wamepokea rushwa yenye thamani ya Sh. milioni 900. Hata hivyo, naye alishinda kesi.

  Je na hawa hata hivyo watashinda kesi ? Ikiwa mmoja mmoja waliweza kushinda kesi je hili genge zima ? Tumesikia wakubwa wakisema kuwa watu wanaohusika ni hatari au kasheshe la safari hii ni hatari kudili nalo ,je kwa kuanza kufikishwa mahakamani ndio tuamini kuwa hatari ambayo wakiiogopa au wakiisema ndio imeshadhibitiwa. Tatizo tumepelekwa kwenye EPA wakati kuna majanga ya ubadhirifu ambayo inaonekana kutaka kufunikwa na hili la EPA ,ni lazima wananchi waamke ,mahakama kunaweza kuendeshwa kesi tofauti kwa wakati mmoja ,tunataka wadau wadai na kesi zingine za ubadhirifu zianze kunguruma , hakuna kulala mpaka kieleweke.Ndio utawala bora ulivyo ,ni madai tu.

  Kwa kukumbusha tu kuna majina ambayo tulikuwa tukiwasikia wakubwa kuwa wanayo ,majina ya wale watu wa unga ,naona tatizo limezimika ghafla na hatuwasikii tena , wabunge mnayo kazi ya kuwakumbusha viongozi wamefikia wapi na listi ya majina ya vigogo wa unga.
   
Loading...