Just relax ndugu, interview siyo vita

Just relax ndugu, interview siyo vita

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,383
Reaction score
1,360
Kuna watu humu ndani huwa wanatoa ushauri mbali mbali kuhusiana na namna ya kufanya interview lakini wanasahau kuwashauri watafutaji wa kazi kuwa interview siyo vita kama vya Kagera enzi za Idd Amin.

Mtu unaenda kwenye interview huko unakutana na watahiniwa wenzako basi wewe unanuna kama unauza sumu,hutaki kushare hata idea moja ama hata kusalimia wenzako wenzako unaowakuta pale kwenye bench la kusubiria inakuwa issue.

Basi nakuomba badilika ndugu yangu ukifika pale jichangamshe salimia hata mtu mmoja ambae unaona atleast mnaendana then chukua hata contact zake in case kama akipata yeye atakujulisha ili uitoe kazi hiyo kichwani mwako ama pia mtu huyo anaweza akapata na huko alikotoka kukawa nafuu kwako akakuunganisha huko.

All in all interview kama hujui ukiitumia vizuri nayo inakusaidia kutengeneza network.

Nasema hivo kwa sababu mimi nimepata kazi kupitia kwa mtu niliekutana nae kwenye interview and all I did was just to exchange number then nikamuambia kuwa kama ukipata update yoyote ile ama kama mimi nikipata update ntakufahamisha, then yeye akawa amepata update kabla yangu na kazi kweli akaipata.

Alifanya kazi sehemu ile just one week na kwa kuwa alikuwa ameshaaply sehemu nyingine kikaitika, alichokifanya ni kwenda kwa HR kuwaambia kuwa yeye anaondoka kwa kuwa amepata his dream job then you know what he did ni kunirecomend mimi kuwa ananifahamu vizuri na akawahakikishia kuwa I can deliver very well.

Hivi navoongea nipo nachapa mzigo. Kwa hiyo ushauri wangu usiende kwenye interview kana kwamba unaelekea vitani Darfur Sudan, share idea na kuwa muwazi ulipo
 
Hahahaa sure mkuu Kuna watu huwa wananuna hata hawasalimii hawajui kuna maisha mengine baada ya hiyo interview!
 
Ni kwel ndugu yangu hasa kwa wale watu unakuta wana vimemo pale ndo huwa wananuna na kujifanya wapo bize hata kuwaacha wenzao kwe bench na kuzunguka kwa hao wanaowafahamu hapo ofisini.kwel inakera.
 
Back
Top Bottom