Jussa kuwasilisha hoja binafsi BW

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
MJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa, amewasilisha kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi, taarifa ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi.
Hoja binafsi hiyo inaomba Baraza la Wawakilishi kupitisha Azimio la kuitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kuchukua hatua za kuandaa mapendekezo ya mambo ya msingi, ili yazingatiwe kwenye utaratibu wa kuandaa Katiba Mpya ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Jussa alieleza kuwa hoja hiyo imelenga kutumia Kanuni ya 27(1)(m); 27(3); 47(2); 48(1) na 49 (1) ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi (Toleo la 2011).
Jussa alisema hiyo inatokana na hatua iliyofikiwa baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, katika hotuba yake kwa Taifa aliyoitoa Desemba 31, mwaka jana, kutangaza kusudio la serikali kuchukua hatua zitakazopelekea kuandikwa kwa Katiba mpya.

Alisema kutokana na hatua hizo, ameona kuna haja ya kuomba Baraza la Wawakilishi kuchukua hatua ya kutoa azimio litakalotoa muongozo kwa SMZ kuweka mambo ya msingi, ambayo Zanzibar ikiwa mojawapo ya nchi mbili zinazounda Tanzania, inapaswa iyawasilishe ili nayo yazingatiwe.

Jussa alisema yanatakiwa yazingatiwe wakati huu serikali ikiwa inaandaa Muswada wa Sheria utakaopelekwa kwenye Bunge la Aprili."Naamini kabisa SMZ ikiwa ndio yenye kushikilia dhamana ya uongozi wa Zanzibar na inayowakilisha maslahi, matakwa, matarajio, haki na wajibu wa wananchi wa Zanzibar, ina wajibu wa kutayarisha mambo hayo ya msingi ambayo Zanzibar kama mshiriki mmojawapo wa muungano inataka yazingatiwe,” alisema na kuongeza:

“Yaingizwe katika mfumo mzima wa utaratibu wa uandaaji Katiba mpya ya Tanzania na ambao unapaswa kusimamiwa kwa pamoja na pande zote mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
 
Back
Top Bottom