Juni 05: Siku ya Mazingira Duniani (World Environment Day)

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
KUHUSU SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

Tangu mwaka wa 1974,Siku ya Mazingira Duniani  huadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni, hushirikisha serikali, mashirika ya biashara, na raia ili kushughulikia masuala nyeti kabisa ya mazingira.

KAULIMBIU:
Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani katika mwaka wa 2022 yataendeshwa chini ya kaulimbiu Dunia Moja Tu, na inatoa wito wa kufanyia marekebisho sera na maamuzi yetu ili kuwezesha kudumisha usafi, kutochafua mazingira na kuishi kwa njia endelevu na mazingira. Sayari hii ndiyo makaazi yetu tu, na ni sharti tulinde rasilimali zake zinazoweza kuisha. Dunia Moja Tu ilikuwa kaulimbiu ya Kongamano la Stockholm la mwaka wa 1972 lililopelekea kuanzishwa kwa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP). Miaka 50 baadaye, dunia inapoendelea kushuhudia changamoto za aina tatu duniani za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, uchafuzi na taka, mambo yanayoendelea kuhatarisha sayari yetu, kaulimbiu hii bado ina mashiko.

JAMII
La muhimu zaidi, Siku ya Mazingira Duniani ni jukwaa la kimataifa la kuchombea mabadiliko chanya. Hutoa msukumo:
  • kwa jamii kutafakari upya kuhusu jinsi inavyotumia rasilimali za Dunia zinazoweza kuisha
  • mashirika ya biashara kubuni mifumo isiyochafua mazingira na kukuza chumi zisizochafua mazingira
  • wakulima na wazalishaji kuzalisha kwa njia endelevu
  • serikali ziwekeze kwa uboreshaji wa mazingira
  • walimu kushawishi wanafunzi kuchukua hatua, na
  • vijana kukuza hatima endelevu.
MWENYEJI
Kila mwaka, maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani husimamiwa na nchi tofauti inayoendesha maadhimisho rasmi. Mwenyeji wa mwaka wa 2022 ni Uswidi.

Chanzo: UNEP (Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa)

VITU UNAVYOWEZA KUFANYA KUTUNZA MAZINGIRA


1) Epuka Kutupa Taka Ovyo: Badala ya kutupa takataka barabarani au sehemu nyingine kinyume na taratibu, jenga tabia ya kutupa taka sehemu husika

2) Jenga Tabia ya Kutumia Vitu zaidi ya Mara Moja: Kila inapowezekana, jitahidi kutumia Bidhaa zako (Mfano Mifuko rafiki isiyo ya plastiki) mara kwa mara badala ya kuitupa

3) Tunza Maji: Usiache bomba wazi kama huna matumizi na maji. Watu wengi huwa na tabia ya kuacha wazi bomba ya kupoteza Maji bila sababu

4) Panda Mti: Jielimishe wewe na kuwaelimisha wengine kuhusu Mazingira na vitu vya kufanya ili kuyalinda
 
Ahsante sana kwa Elimu nzuri. Bila Mazingira sisi tunakua hatuna utofauti na 'Wanyamapori hai' pamoja na viumbe wengine.
 
Kariakoo inaongoza kwa uharibifu wa mazingira,
Kuna binadamu wanakojoa barabarani kama wanyama au zaidi ya wanyama,
Mambo ya mazingira tuwaachie wenyewe sie bado sana,
Na mamalaka zipo na zinaona kimyaaaa
 
Back
Top Bottom