Uzuri ni kwamba hawa waarabu, waajemi, wazungu+wazayuni, wahindi, na wachina wanajua wanapambania nini ktk migogoro yao, na wanajua mipango yao na target zao, pia wanajua suluhisho la matatizo yao, tofauti na sisi waafrika wapumbavu ambao tunaendeshwa kwa mihemko kufuata migogoro ya hawa watu na kuifanya kama yetu.
Kwa miaka na miaka hawa watu hasa waarabu, wazayuni, waajemi na wazungu wamekuwa wakitumia mgongo wa dini kama catalyst ya migogoro yao, yaan migogoro yao wameiweka ktk roadmap ya matukio ya kihistoria yaliyopita na ubashiri wa mipango yao ijayo kuiita UNABII kupitia vitabu vya kipropaganda (biblia, Quran, Tanakh), then sisi wapumbavu tusiopenda mambo yetu na kudandia mambo ya watu tunawaona wanaakili sana huku tukiabudu historia zao na mipango yao tunayoaminishana misikitin na makanisani tukiita UNABII.
hawa wazayuni na wazungu wanavyotwangana dhidi ya waajemi na baadhi ya waarabu hapo middle East ni plan zao na migogoro yao ya zamani na mipango yao ni kila mmoja kutanua utawala&ushawishi wake hivyo anatumia kila aina ya njia/siraha kutimiza agenda zake.
Huwa nafurahi kuona kuna waTanzania wanaoijua vzr historia na kutambua propaganda tunayolishwa kuhusu hii migogoro tuliyoaminishwa ni ya kidini+kiimani kumbe si kweli ni muendelezo wa tamaa za madalaka na ushenzi wa kumtawala mwingine hakuna habari za Mungu wala imani hapo.
Back to topic, hao waajemi(iran) wanajua hasa wanapigana na watu wa aina gani ndiomaana wanakaza kutumia sana akili ili kujilinda na kutimiza plan zao huku wakizuia ama kuchelewesha plan za adui wao, wanajua kabisa adui wanayepambana nae ndoto yake ni kupanua utawala mpka maeneo yao na kuweka sheria zake, huku na wao wakitumia ubabe wa historia yao kuendeleza nguvu zao kuzuia kuanguka.
Waafrika hasa ninyi wafuasi wa dini, jifunzeni kusoma mambo nje ya imani na dini zenu, kuna mengi mnayakosa kwa kukataa/kupinga kisa hayafurahishi nafsi zenu sababu yanakosoa na kugusa imani zenu.
Historia hujirudia na ukweli hubaki kuwa ukweli haijalishi unaumia au kuukataa unabaki kuwa ukweli.
Waafrika tunatumika tu kusapoti propaganda na migogoro ya watu weupe huku tukijichelewesha wenyewe kufanya maendeleo kisa huu ushabiki wa hizi pande za watu weupe.
Wafuasi wa dini tumieni akili mahala panapohitaji facts& knowledge na sio hisia na mihemko yenu ya mahaba mliyolishwa makanisani/misikitin.