Jumuiya ya Kimataifa ya Uchakataji Nafaka (IAOM)

Jumuiya ya Kimataifa ya Uchakataji Nafaka (IAOM)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema serikali itaendelea kuhakikisha ina imarisha sekta ya uchakataji wa bidhaa za nafaka Zanzibar.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa 32 wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uchakataji Nafaka(IAOM) uliofanyika Hoteli ya Verde iliopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk.Mwinyi amesema serikali inatambua mchango wa sekta hiyo ya Uchakataji wa bidhaa za nafaka nchini.

Mbali na hilo, amesema mabadiliko ya tabia ya nchi yameathiri uzalishaji na Uchakataji wa bidhaa za nafaka hivyo amewataka wadau wa mkutano huo kujadili suala hilo na kupata ufumbuzi wake.

Amesema mkutano huo utawasaidia wadau hao katika kubadilishana uzoefu, uelewa na teknolojia kwenye sekta ya uchakataji wa bidhaa za nafaka.

Pia, Rais Dk. Mwinyi amewaalika wadau hao kuja kuwekeza Zanzibar hususan katika eneo la uchumi wa buluu.


[emoji414] 26 Oktoba 2022

[emoji625]Hoteli ya Verde, Zanzibar.View attachment 2399128View attachment 2399127

IMG-20221027-WA0013.jpg
View attachment 2399129
 
Back
Top Bottom