Jumeirah Beach (Dubai)imejawa na hoteli nyingi sana za nyota tano japo inayojulikana kuliko zote ni Burj al arab (pichani),hapo ndipo Osterbay +Masaki ya Dubai mbali ya hoteli kuna nyumba nyingi sana za mafisadi,Kama mafisadi wanavyoficha pesa Switzerland ndivyo wanavyojenga majumba Dubai (hasa Jumeirah beach)viongozi wengi waliopinduliwa au kukimbia nchi zao wanaishi hapo mfano Benazir Bhuto (baada ya kupinduliwa alipokuwa waziri mkuu wa Pakistan -RIP).Thaksin Shinawatra (aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand) na Perez Musharaf (aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan )hawa ni wachache tu lakini ni viongozi wengi sana waliojenga nyumba na hoteli katika beach hiyo.Zaidi ya hao (mafisadi)watu wengine wenye pesa kama Tiger Woods,Beckham nk wamejenga pale.Serikali ya Dubai walichofanya ni kuandaa mazingira mazuri sana (security)kwa wezi na ndio wamewekeza biashara kubwa sana hasa za hoteli mjini hapa.
Kaka nashukuru kwa ufafanuzi mzuri.
Kwahyo unataka kusema soon dubai itakuwa Tax Heaven?
Mkuu Bavaria, Naona unafanya shopping ya Tax Haven. Singapore wanakusuburi... Hahahaha
Mkuu huwezi kuweka mayai yote kwenye kapu moja kaka.
Nimewasiliana na bank za Cayman, Luxemborg na Mauritius, wamenipa huduma wanazotoa. Bado nipo kwenye window shopping hadi nitakapo fanya maamuzi ya mwisho.
Mkuu Bavaria. You are making a wise business decision.
Citibank Hong Kong pia wanafungua account kirahisi na huhitaji kuwaona, ni online application. Kama unafanya biashara China inasaidia, unaweza kufungua kwa Yuan, Yen, U.S. dollar au Pounds. Wanakuletea ATM / credit card by fedex.