Cliffhanger
JF-Expert Member
- May 22, 2018
- 721
- 1,294
Siku ya Jumapili kule kijijini kwetu ilikuwa ndio siku ya "show off"; hii ndio ilikuwa siku ya kuvaa vizuri. Kabla utaratibu wa kuwafuata waumini walipokaa ili watoe sadaka, wale watanashati wa kijiji tulikuwa tunakuwa wa mwisho kuinuka kwenda kutoa sadaka. Hiyo yote ilikuwa mbinu ya ku attract attention ya warembo wa kijiji.
Ila jambo ambalo lililokuwa likinishangaza sana ni wale wazee ambao walikuwa wanaogopwa kijiji kizima kama wachawi wakubwa; ndio waliokuwa wa kwanza kufika kanisani na viti walivyokuwa wanakaa ni vile vya mbele kabisa.