Jumanne Muliro kumrithi IGP Sirro?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Mzee Sirro amekaribia kustaafu, kwa nidhamu na maendeleo ya Jeshi la Polisi sisi tunaofuatilia utendaji wa Ma RPC tunaweza kusema Muliro atachukua nafasi ya Sirro.

Kwa namna alivyotuliza Mwanza, kwa alivyofanya kazi DSM na kwa anavyojiamini kwenye kujenga hoja natamani kuona yeye au watu wa aina yake wakikabidhiwa Jeshi kuliko kuwakabidhi aki Mroto au Mambo sasa
 
Uuuwiii ,,,,,Jamani tutakuwa tunamuundia majungu IGP Sirro

IGP aliepita kwa heshima Said Mwema aliongezewa muda na JK kama miaka minne mbele baada ya umri wa kisheria wa IGP Mwema kustaafu kufika

Na pia hata Mambosasa ni Afisa kamishna wa Polisi mchapakazi sana , ni ngumu kumpata mtu kama Mambosasa (uchapakazi ni tabia adimu sana kwa sisi binadamu wenye ngozi nyeusi) kwa hiyo naomba tusimuundie majungu nae

IGP Sirro kama akiongezewa muda kama alivyoongezewa Said Mwema basi atastaafu mwaka 2027
 
Hao wote mlio wataja hapo vyeo vyao ni vidogo sana vya kuteuliwa kuwa IGP maana kuna vyeo viwili juu yao DCP na CP bila shaka kuna watu wenye vyeo hivyo tajwa hapo juu wanasifa za kuwa IGP. Ila yote kwa yote hongereni kwa kuwapigia debe washua wenu waje kuwa ma IGP.
 
Na yeye ni Mzee karibia ku staafu
 
Mambosasa analea jambazi anafahamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…