Juma Nkamia amesoma wapi Uandishi wa habari?

Juma Nkamia amesoma wapi Uandishi wa habari?

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
JUMA Nkamia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini (CCM). Kabla ya hapo alikuwa msoma habari na mtangazaji wa mpira katika Shirika la Habari la Taifa (TBC) na baadaye mashirika ya nje ya BBC na VOA.

Kwa utambulisho huo inamaana Nkamia ni mwanafamilia mwenzetu katika tasnia ya habari, japo matendo yake sasa tangu achaguliwe kuwa mbunge yanaonesha kuwa uandishi wa habari haujui au kasahau.

Nkamia amekuwa mtu wa kubwatuka bungeni na kuwasema vibaya waandishi wa habari kana kwamba ni watu masikini, ombaomba wenye kuburuzwa na matajiri kuandika uongo dhidi ya serikali.

Kila akipata nafasi bungeni kuuliza swali kwenye wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, Nkamia anahoji ni lini muswada wa habari utaletwa bungeni ili kuwadhibiti waandishi makanjanja wanaotumiwa.

Nkamia amefika Ulaya na Amerika kikazi lakini si kweli kwamba hiyo ni sababu ya yeye kujua sana mambo kuliko wanahabari wengine. Ziko sababu nyingi za kufika huko yawezekana hata ikiwa walivutiwa na sauti yake tu.

Lakini tangu amekuwa mbunge Nkamia amekuwa na mtazamo hasi kwa tasnia hii. Anaiona ni ya watu wasiojua, wasio na maadili, wasiolipwa mishahara minono, wasioajirika na mengine mengi.

Kwa uelewa wake huo, kwenye Bunge la bajeti lililopita wakati wa kujadili hotuba ya Wizara ya Habari, Nkamia alilituhumu Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri kuwa vyombo hivyo vilivyoanzishwa kwa masilahi binafsi ya watu.

Nikiri kwanza kuwa Nkamia hana viwango vya kumjadili kwenye safu hii ya fikra mpya lakini kutokana na kituko alichokifanya wiki hii bungeni nalazimika kumleta kwenu tushauriane masuala kadhaa dhidi yake.

Baada ya wapinzani kutoka nje wakisusia mjadala wa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, Nkamia alikuwa miongoni mwa wabunge wengi wa CCM waliochangia hoja bila kujielekeza kwenye hoja husika (wapiga kelele).

Kwa dakika zake kumi alitumia takribani dakika tano kuonesha umbumbu wake kwenye tasnia ya habari kwa kutojua habari ni ipi kwa wanahabari makini.

Mbunge huyo alianza kwa kujitapa kuwa amefanya kazi ndani na nje ya nchi kwenye mashirika makubwa, kwamba hajawahi kuona wanahabari wa ajabu kama hawa wa Tanzania.

Nkamia akadai kuwa wakati wapinzani wanatoka nje vile vile wanahabari wote waliondoka ukumbini na kuwafuata huko nje. Kwa upeo na maono yake wapinzani hawakuwa na habari bali habari ilikuwa ndani kwa wabunge waliobaki ukumbini.

Akaongeza kuwa kama wamekimbilia kwa wapinzani wataandika taarifa wala si habari. Huyu ndiye mwandishi anayejiita nguli kwenye tasnia, alifanya kazi Ulaya za kusoma habari na kutangaza mpira.

Mpaka naandika safu hii sijamuelewa Nkamia alikuwa analenga kusema nini kwamba habari za kuwapelekea Watanzania ziliachwa ndani ya Bunge halafu wanahabari wanakimbilia nje kuwahoji wapinzani.

Muswada ulisomwa, wabunge wa CCM wakaupigia makofi kwa ishara kwamba wanakubaliana na kile kilicholetwa na serikali yao. Walipoanza kuujadili hakuna aliyejikita kwenye vipengele badala yake wakaanza pongezi, kejeli, kashfa na matusi ya nguoni kwa wapinzani.

Sasa pengine Nkamia kwa uzoefu wake wa kufanya kazi ndani na nje ya nchi, aliona habari ilikuwa wapi hapo ya waandishi kuandika wakati wananchi walikuwa wanataka kujua hasa sababu za wapinzani kutoka nje na kuacha kujadili muswada.

Kimsingi kote kulikuwa na habari lakini zaidi nje walikokwenda wapinzani ndiko kulikuwa kwa muhimu sana kwani wananchi walitaka wajue wawakilishi wao huko walikokwenda imekuwaje.

Na hii ilikuwa ni kazi ya kufanywa na TBC1 ambayo ndiyo inaonesha vikao hivyo moja kwa moja. Lakini kwa utashi wao pengine na maelekezo ya wakubwa waliishia kutuonesha meza ya spika na mawaziri.

Kumbe ulikuwa ni wakati muafaka kwa wanahabari makini kukimbia nje upesi na kuzungumza na wapinzani kupata sababu za msingi zilizowatoa nje pamoja na hatua wanayokusudia kuichukua.

Lakini Nkamia alituambia hiyo ni taarifa si habari. Sipendi kuhoji mwalimu wake kama alimwelewa ila nahoji alikosoma uandishi wa habari kiasi cha kushindwa kutofautisha habari na taarifa.

Kama ilivyo kwa wabunge wengi kutaka wapigiwe makofi wakati wa kuzungumza nadhani hata yeye baada ya kuona hana hoja ya kuchangia kwenye muswada ule aliamua kuwashambulia waandishi ili apigiwe makofi.

Yawezekana Nkamia ni mwanahabari kweli lakini kama matatizo ya wanahabari wenzake hayajui ni vizuri akajielekeza kuzungumzia kero za wapiga kura wake kama wanavyofanya wanahabari wenzake, Ester Bulaya na Lucy Mayenga, ambao wameamua kujiweka mbali na wanahabari. Tafakari!

Kwa maoni yangu
Hii kauli ya Nkamia nadhani inatafuta cheo mahala.Tukae tusubiri kama hata zawadiwa wizara hiyo ya kubana magazeti na waandishi.

Aliingia fomu 6 RTD baadae nadhani alipewa shavu kwenda kusoma.Ni kama walivyo kina Gerson Msigwa na Benjamin Rwegasira.
 
Juma Nkamia ni kilaza, huyu si alishawahi kusema Jamii forum ifungwe? Hakika wana Kondoa walichagua kituko.
 
Nkamia sio mtu makini kabisa. ni kama anajipendekeza kwa kikundi flani vile
 
hahahahaha wanahabari wakiambiwa ukweli wanapayuka hao haya tuone utashi na umahiri wa mwanahabiri huyu.nachojus nkamia ni mkongwe kwenye habari bila kujali alikwenda ulaya hakwenda au amesoma times journalism au hakusoma ambako umesoma wewe mtoa taarifa unaejiita mwanahabari
 
Alisoma wakati wa ujima, harafu shule za wakati huo ilikuwa n kukaririshwa, so in the really journalism sense it doesn't apply.
 
kilaza tu huyo na mlamba viatu vya wakubwa kutafuta cheo, hana hoja wala mantiki ktk uchangiaji wake bungeni.

ni limbukeni mkubwa tu na nakumbuka vizuri pindi katoka uingereza sijui alikuwa na shughuli gani huko kama si kibarua wa part time wa bbc kwa kutaka kujifanya anatangaza matangazo ya mpira hapa nchini kwa lugha ya kiingereza asichokijua.

ni mtu wa kujitongozesha kwa wakubwa, mtaolewa wengi tu kwa staili hizo kwani mkeo ajitongozeshe na wewe pia.
ajabu!!!

anatia kinyaaa huyo hamnazo.

ni kubwa lkn ni jingajinga fulani hivi.
 
Kweli mkuu huyu bwana anaonekana kujipendekeza sn kwa wakubwa ili apate cheo.mm naona wana kondoa walichagua janga.
 
huyu ni mtangazaji wa mpira,angejiuliza iwapo mpira utatoka nje ya uwanja utaendelea kuwataja tu wachezaji mpira waliobaki ndani ya uwanja au atashughulika na anayefuata mpira nje kuurudisha uwanjani?pia kaz yake nmi kusoma habari na kutudanganya kwa kutangaza mpira tofauti na kinachotokea uwanjani
 
wanahabari na nyinyi acheni kujiuza kama malaya wa Mrina, leo Mh. Peter Msigwa ameripoti kwa majina yao baadhi ya wandishi wa habari waliowekwa hotelini na kupewa hela na mmoja wa mawaziri wa maliasili na utalii ili waripoti kuwa anahongwa na mafisadi awatetee ktk kazi zao.
 
Juma Nkamia ni kilaza, huyu si alishawahi kusema Jamii forum ifungwe? Hakika wana Kondoa walichagua kituko.

Tangu huyu jamaa aseme ""<Naongea na mwenye mbwa siongei na Mbwa>""Niliwadharau waliompigia kura (kondoa kusini).Najiuliza wanakondoa ni nani aliyewaloga?.

Huyu jamaa ni kilaza,huwezi amini mtu akitoka kwenye familia maskini anabadilika hivi.

KONDOA KUSINI MPOOOOOOOOOOOOO?


KONDOA KUSINI MPOOOOOOOOOOOOO?


KONDOA KUSINI MPOOOOOOOOOOOOO?
 
Back
Top Bottom