Juma Duni: TANESCO inaendeshwa kwa rasilimali za Muungano ikiwa ni pamoja na kodi kutoka Zanzibar

liljeff87

Senior Member
Jan 3, 2016
174
85
Magufuli wakati unataka Umeme Zanzibar kwa deni la billioni 121 tunakukumbusha kuwa TANESCO inaendeshwa kwa raslimali za Muungano ikiwa ni pamoja na kodi ya mapato kutoka Zanzibar mbali ya madeni mengine tunayoidai Tanganyika.


Bahati njema Bodi ilipeleka Paundi za kiingereza 82,840 kama ni mchango wa Zanzibar katika uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania. Fedha hizo zilimezwa na Tanganyika na kuundwa Benki Kuu moja, The Bank of Tanzania (BOT) kwa mtaji wa Paundi za Kiingereza milioni moja wakati huo ikiwa ni sawa na Shilingi milioni ishirini (20,000,000) za Afrika Mashariki (East African Shillings) Kasoro ya kufikia pauni 1,000,000 ilijazwa na Serikali ya Muungano. Kwa urahisi zaidi tazama hesabu hizi chini:

Mchango wa Serikali ya Tanganyika ni Pauni za Kingereza £668,884

Mchango wa Serikali ya Zanzibar ni Pauni za Kingereza £82,840

Jumla ndogo (ST + SMZ) ni pauni £751.724

82,840*100 /751,724 = 11.025%

82,840 *100/668,884 = 12.388482%

Muda wote ule wa uhai wa EACB, Zanzibar ilikuwa ikipata si chini ya asilimia 12.40 (12.4 %) ya mgao wowote ule unaotolewa na Bodi kwa Tanganyika. Ukweli huu unathibitishwa kwa kuangalia mgao uliofanyika wakati zikigawiwa fedha za mwisho zilizobaki katika Account za Bodi hiyo kama zilivyooneshwa katika kumbu kumbu ya Bodi hiyo za (21st August 1972 zilizoandikwa na Mr. A.C.C.Roberts)

Chanzo : Juma Duni.
 
Tatizo hapa ni mhusika wa hili saga kutokujua hata Jinsi muungano ulivyo!!! Kata umeme tuvunje muungano!!! Jino kwa Jino!!! Kupelekesha watu wapelekeshe watanganyika wenzio sisi tangu enzi za Karume senior hatukuwahi kumbembeleza mtu!! Muungano ni kama koti tu likikubana unalivua!!!
 
Walipe tu.mie nashangaa tunakuwa na double taxation ukinunua vitu zenji ukifika bandari unalipa kodi tena.

mkuu hiyo ni moja ya tatizo la muungano .. yaani gari unaitoa dubai kwenda znz kodi nafuu lkn ukitoa znz kuja dar kodi yake ujumlishe hela ulonunulia gar + na kodi ulotoa znz na nyengine zitaongezeka.. ndio utaitoa bandarini vituko aisee
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Tatizo hapa ni mhusika wa hili saga kutokujua hata Jinsi muungano ulivyo!!! Kata umeme tuvunje muungano!!! Jino kwa Jino!!! Kupelekesha watu wapelekeshe watanganyika wenzio sisi tangu enzi za Karume senior hatukuwahi kumbembeleza mtu!! Muungano ni kama koti tu likikubana unalivua!!!
Hoja iliyopo hapa umeme ulipwe maisha yaendelee kama kawaida, hii awamu nyingne tunataka maendeleo tu
 
HAKUNA CHA BURE, WALIPE AMA WASIPOLIPA WAKATIWE UMEME, HAIWEZEKANI SISI TUNAOLIPA BILI TUNAPATA UMEME KWA MGAO.
KAMA VIPI WAKATE NA WANYOFOE MPAKA NYAYA ZETU, WADAU KIBAO WANAHITAJI UMEME MKURANGA HUKU
 
Sawa,Wazanzibari wanalipa bills zao,je makusanyo ya kodi hizo zinapelekwa wapi hadi deni liwe la miaka 20 tena zaidi ya 120bln? Wanakula watu wachache?


Hawa jamaa watu wa ajabu. Kule kuna kitu kinaitwa ZECO (sawa na TANESCO) hawa jamaa wanapata umeme toka bara kisha wao wanawauzia Wazanzibari!

Fullscreen%20capture%2002042014%20122034.jpg


President Ali Mohammed Shein has directed the Zanzibar Electricity Company (ZECO) to improve its services and strengthen revenue collection from its customers."Be tough on bill payments and collection of debts. All your customers including my office (State House) must pay bills. Short of that, disconnect power," said Shein when inaugurating power in Ukunjwi Village, north Pemba.He said that ZECO is responsible for providing best services alongside curbing bill evasion and people connecting electricity illegally should be arrested and charged.Shein said that electricity is now prerequisite for development and that people need power supply all the time
 
SIJAELEWA HII NI HESABU GANI???....maana hiyo gawanya hapo imenichanganya
Jamaa ww hujui hesabu kweli teh teh. Katika hesabu za kuzidisha(sehemu/fraction) haijalishi denomenator iko upande gani jibu ni lile lile(haswa kama hii ya kutafuta asilimia)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom