Julius Mtatiro@ Clouds 360: Lipumba alikuwa CUF kimkakati zaidi

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Akihojiwa katika kipindi cha televisheni cha Clouds 360 asubuhi amesema Lipumba kwa muda mrefu amekuwa CUF kukihujumu chama hiko.

Amedokeza katika mgogoro wa CUF , CUF haipambani na Lipumba peke yake bali nyuma ya Lipumba kuna dola na serikali kwani ingekuwa CUF inapambana na Lipumba peke yake mgogoro ungekwisha maapema.

Aelezea jinsi Lipumba alivyokuwa na ushawishishi mdogo kwa bodi ya wadhamini kwani anaungwa mkono na wajumbe wawili wa bodi ya wadhamini kati ya wajumbe Tisa.

Asema serikali inamtumia Lipumba kuvuruga CUF, kwa kuhofia nguvu za CUF.

Migogoro inadhoofisha vyama vya siasa lakini vile vile inaimarisha vyama.

Lipumba aliondoka CUF ili kudhoofisha chama, lakini badala yake chama kimepata nguvu kwa kuweza kupata uongozi wa nyadhifa mbalimbali

Lipumba hana ushawishi katika chama, alipokuwa mwenyekiti bara ulikuwa na wabunge 0 baada ya kuondoka chama kimepata wabunge 15.

Hata CHADEMA kilihofia CUF baada ya kuzidi kukubalika bara.

Ushirikiano wa vyama vya upinzani ni msingi mkubwa kuleta demokrasia nchini baada ya kuua vyama vya siasa.

Maoni ya wanachama iwapo Lipumba akiwa mwenyekiti wataondoka katika chama.

Lipumba anasafiri na watu katika ziara mbalimbali kwani katika ziara zake hupata watu wachache wanaofika 15.

Atoa mfano ziara ya Lipumba Luangwa Lindi Lipumba alikosa watu, ilibidi mkuu wa wilaya ashawishi wanachama wa CUF wamsikilize Lipumba.
 
Mwongo huyo alipokuwa mwenyekiti Cuf ilikuwa na wabunge Wawili bara Baruwani yule Albion, na yule anayejiita Bwege, sasa kutoka mbili mpaka unasema zero ukiwa unajua ukweli je hayo mengine tutakuamini mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe....
 
Kukaa na familia ni kitu muhimu sana kwa kiongozi,lakini kukaa peke yako unakuwa upoupo tu.Lipumba pamoja na umri wake,usomi wake lakini kiukomavu wa maamuzi ,Lipumba bado ni mtoto au kijana.Ni morani au mubalanda kikwetukwetu
 
Sasa mkuu katika mazingira ya kawaida kuna tofauti ya 2 na 0? Hasa ukizingatia amegombea urais mara 4 mfululizo?
 
SIJAWAHI KUONA MTU WA AJABU KAMA MTATIRO KATIKA DUNIA HII .......

BADALA YA KUJIPANGA KWA AJILI YA UBUNGE 2020 JIMBO LA SEGEREA ILI ASHINDANE NA BONA WA CCM YEYE ANAPAMBANA NA LIPUMBA WAKATI ANATAMBUA KESI IKO MAHAKAMANI
 
Kukaa na familia ni kitu muhimu sana kwa kiongozi,lakini kukaa peke yako unakuwa upoupo tu.Lipumba pamoja na umri wake,usomi wake lakini kiukomavu wa maamuzi ,Lipumba bado ni mtoto au kijana.Ni morani au mubalanda kikwetukwetu
Mwongo wewe. Lipumba ana mke. Au ulitaka uolewe wewe
 
Serikali inawaingilia au katiba yenu wenyewe..??ni wehu tu kuikana katiba yenu..kama anatumika alipokuchagua kutumikia chama mbona hukukataa..punguza mwili huo walau upate akili.
 
Mtatiro Na genge lake wote akili zao haziko Sawa baada Lipumba kuandika barua ya kujiuzuru nini kilichowazuia kuithibitisha mapema ili kutimiza takwa la katiba yao ndio Lipumba alipoona hawataki atoke akaamua kurudi kwenye nafasi yake saiz wanalalama kwenye media
 
Mwongo huyo alipokuwa mwenyekiti Cuf ilikuwa na wabunge Wawili bara Baruwani yule Albion, na yule anayejiita Bwege, sasa kutoka mbili mpaka unasema zero ukiwa unajua ukweli je hayo mengine tutakuamini mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe....
Hana haki huyo. Atupwe Kolomije tu akalime
 
Mtatiro kiongozi wa Facebook bakia huko huko Facebook uendelee kufakamia likes. Chama cha watu hicho we kafiri umejipachika tu. Wenyewe wakipatana we mgeni huna chako. Afadhali uende NCCR kwa Wagalatia wenzako ukazibe pengo la Mbatia. Na akipona unampisha!
 
Kwani Mtatiro yeye Nyumbu!
 
Back
Top Bottom