Julius mtatiro aeleza kinachomkera cuf

Julius mtatiro aeleza kinachomkera cuf

Julius Mtatiro amefanya mahojiano na gazeti la Mwanahalisi na kusema kinachomkera na kumuumiza roho ni dhana iliyojengeka kwamba CUF ni chama cha Kiislamu.Amepinga vikali dhana hiyo na kusema hakuna upendeleo wowote wa kidini ndani ya CUF na ndio maana yeye Mkristo akapewa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.Amesema ataanzisha moto nchi nzima kudai katiba mpya na kufuta hiyo dhana ya udini dhidi ya chama chake.Amesema atahakikisha ule umaarufu wa kale wa CUF utarudi na chama chake kitavipiku vyama vyote hapa nchini.
Wadau imekaaje hii? Kweli Julius Mtatiro ataweza kufuta dhana hii....................
Ni kwel huo ndio uvumi ulioenea kuhusu vyama hivyo viwili lakn yaan cuf-uislam na chadema ukiristo k2 ambacho hata mimi kinanikera sana kwa wa2 kushndwa kujua kuna m2 mwenye dini na kuna chama cha msingi hapa 2siangaike na imani yake bali kama umependa sera za chama hucka jiulize je? Anazitekeleza sera zilizo andikwa?
Pili jua kwamba hii imekuwa ni mtaji kwa viongozi wa chama cha sisiem pale wanapohisi kushindwa wala kwa wananchi tatizo co kubwa kihiv.
Mtatiro anaweza lkn nadhan anaweza kushndwa kwa ajiri ya resourses in general namtakia maandaliz na utekelezaji mwema.
 
Mkuu,

Hongera sana, naona urefu wa I am full time……..umepungua. yale mengine umepitisha uamuzi mzuri wa kuyaacha.
Hongera sana mkuu na hili lililobaki litaondoka!
well done, Rev.

Mkuu inaoneka wewe huna kipya unapenda fatilia nonsensical issue unaweza shangazwa ukingundua Rev Masanilo wa JF ni ustaadhi hata pombe hajawahi iona!
 
Mkuu inaoneka wewe huna kipya unapenda fatilia nonsensical issue unaweza shangazwa ukingundua Rev Masanilo wa JF ni ustaadhi hata pombe hajawahi iona!

Mkuu ,

Sikuwa na maana kuwa wewe ni mgidaji. No,no..nakumbuka tu hii motto yako ya I am full alcoholic………. ilikuwa refu, mengine yamepotea.

Nilikusudia kukuambia tu kuwa nime-notice umeifupisha, mkuu.

Sikuwa nimefikiria hayo mkuu, pole kwa usumbufu.
 
Hivi Wilfred Rwakatare bado ni kiongozi wa CUF?

Ujue rwakatare alikuwa haendi kanisani kabisa... alipoanza tuu kwenda kanisani basi na CUF wakamfukuza.. Sijui kwa nini lakini yawezekana sio udini labda yeye Rwakatare ndio alileta udini pale kwa kuabudu badala ya kusilimu
 
Julius Mtatiro amefanya mahojiano na gazeti la Mwanahalisi na kusema kinachomkera na kumuumiza roho ni dhana iliyojengeka kwamba CUF ni chama cha Kiislamu.Amepinga vikali dhana hiyo na kusema hakuna upendeleo wowote wa kidini ndani ya CUF na ndio maana yeye Mkristo akapewa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu.Amesema ataanzisha moto nchi nzima kudai katiba mpya na kufuta hiyo dhana ya udini dhidi ya chama chake.Amesema atahakikisha ule umaarufu wa kale wa CUF utarudi na chama chake kitavipiku vyama vyote hapa nchini.
Wadau imekaaje hii? Kweli Julius Mtatiro ataweza kufuta dhana hii....................

dhana ya dini ni ya CCM ukweli ni kuwa CHADEMA ni bara na CUF ni zanzibar tuu.. tusubiri katiba mpya my tanganyika ipewe hadhi kuliko kudharauliwa kama zamani..... Basi CHADEMA tunakula nchi kama tunanawa na mafisadi wooote tunawafunga,, tunabaki CHADEMA na wananchi tuu kuyapiga maziwa na asali za nchi hii... Elimu bure mpaka Phd NGUVU YAKO TUUU.... Kila mwekezaji lazima ugawe kipato wa wakazi wa karibu hapo tuu.. Sheria ya fisadi anyongwe kama China vile... Akii ya nani tutawaacha akina Maalim wakifisid Zanzibar kama alivyozoea na wenzake akina Rashid tuliowatenga kwa kuwa budget ya upinzani na matumizi hata hapakuwa na statement ya matumizi... aliiba saaana... hizo mil 200 kila mwezi za upinzani tutatumia kwa operesheni tuu hakuna kulala... waacheni CUF waendelee na ufisadi wao 20005-2010 walikuwa wakipata mill 99 pamoja na 200mil za kambi ya upinzani lakini wapi???? CHADEMA mwisho wa siku ikang'ara kwa kuwa pale hakuna udini au kusilimu ni kazi tuuu... ukianza kupenda kuwa tajiri kama Zitto kwa kuvuruga chama tunakutimua tuuu
 
Bro can you expound the highlighted quotes! Thanks

Sasa ulitaka ashindane na Azan? mwislamu mwenzake?? unajua CUF imekosa nguvu kwa sababu waislamu waligawanyika wengine CCM na wengine CUF, they had to choose JK for presidential.Mtatiro bila aibu akaamua kushindana na Mnyika , sidhani kama alipenda kutoka moyoni, maana kama ni mwanamapinduzi kweli , basi ingekuwa kumpigia debe Mnyika Ubungon na yeye kama kijana angeenda kwa Azan.

Dini Tanzania inashika kasi na wenye kuiendekeza ndio watakaokuwa wakipata aibu kila siku. Isingekuwa dini, Lipumba angepata kura nyingi sana za waislamu wenzake! ila walimtosa wakaona wampe yakhe, handsome boy JK.

Kama kawaida wakriso hwana hiyana, walikipigia CCM, kuna walikipigia CUF, na kuna waliokipigia CDM, and life goes on...raha ya udini ni wenyewe kuanza kuchapana bakora , siku zinakuja we subiri tu, wakati wa ile migao maustaadhi wana tia ndani, shughuli ipo!!!
 
I have the same feeling that CUF is just a normal political party, It is clear that many follower of this very party have different idea regarding this party, If Lipumba and Seif were serious enough to eradicate this problem, it wouldnt be as it is today. They like and enjoy the idea of their followers that CUF is for Islam. Lipumba did his campaign (2010) in areas where Islams are populated most.

The best way to solve the problem is for Lipumba and Hamad to step down, and some other member to step up.

In politics however how much we can rationalize our reasons still people judge differently, and their judgement have big impact is such a way that it can destroy in areas were it was not supposed to be destroyed.

Not far in future even the top leaders of Chadema need to deal with these problem intelectually not just assuming that people understand...no...is to do exactly as they want even if by using propaganda 'danganya toto' this kind of tactics is well employed in politics anywhere.

Mtatiro you made big big mistake to contest with Mnyika, I wished to have you in the house-Dodoma! You made wrong choice, you were supposed to stand with Azan!! you decided not to because of your secret agenda...

CUF kuonekana ni chama cha kidini, ni kosa la CCM kwa sehemu kubwa na ikiwa imechangiwa na kuingia kwa elements za kidini kutoka chama cha NRA cha Abubakar Ulotu. Utakumbuka kuwa kabla ya 1995, CUF ya James Mapalala na Seif Sharif, kilikuwa ni chama kizuri tu na kilikuwa hakina hisia zozote za kidini. NRA ilipofutwa na msajili kwa kuendekeza udini, islamic radicals kutoka NRA wakasema wanahamia CUF kwa vile ndicho chama kilichokuwa na mgombea muislam japo hakuwa muislam safi sana (wakati ule walidai Lipumba alikuwa hajao), walisema ni bora waingie huko na kukipigia kuliko kuingia kwa Cheyo-UMD, Mkapa-CCM, na Mrema-NCCR. Hata hivyo wenye hisia hizo walikuwa ni watu wachache ambao huwa hawakosekani katika jamii, wakiwa na irrational thinking. Hali kadhalika, kulikuwa na elements za namna hiyo kwa baadhi ya Wachagga wachache kuishabikia NCCR kwa sababu ya Mrema, japo kuna watz wengi walimpenda kama kiongozi mzuri by then. CCM ya akina Kolimba ndio ikatumia Mashushu wakijifanya waslam swafi, wakaingia CUF na kukuza hisia za kidini, wakawa ndio wasemaji wakuu na kuwaeleza wanachama kuwa wanatakiwa wamchague kiongozi Muislam, hivyo hivyo, waliingizia mashushu waliojifanya ni akina Mangi, ndani ya NCCR na wakawa ndio wanaharakati wakuu katika kuhakikisha wachagga wanamchagua Mrema. Hapa lengo la CCM ilikuwa ni kuhakikisha kuwa vyama hivi lazima vionekane kwa jamii kuwa ni vya kidini au kikabila, mwisho wa siku imani hizo zilizopandikizwa na watu wachache na KUCHOCHEWA na MASHUSHU WA CCM ndio zimebakia. CCM ilifanikiwa kwa kuvipakazia hivyo vyama na kwa sasa CUF imebaki ikiaminiwa hivyo, na wapo wachache wanaopenda udini na wanaamini kuwa CUF ndio chama chao, basi wanaelekea huko. Kwa NCCR ni kama kilikufa kabisa baada ya migogoro kibao na sasa ni kama kinaanza upya. Juhudi za kupakazia ukabila sasa zimehamia kwenye chama kingine sasa hivi kinachoonekana ni tishio, ni CCM hao hao ndio wanakuza elements za kidini na kikabila, lengo tu waendelee kutawala.

Siasa ni mchezo mchafu, and I thank God I'm not a politician.
 
Mtatiro wazo lako nizuri sana lakini huna uwezo wa kugeuza misingi iliyo ijenga CUF........na huna uwezo wa kuijenga CUF na kuwa maarufu kama unavyo nadi ushauri wangu ondoka CUF mapema kabisa kajiunge na kafulila NCCR mwaka 2015 uta weza kubahatika kupata ubunge sio huko uliko. Na usijaribu kuja CDM kwasababu tumesha acha kupokea mamluki shibuda anatutosha

hapo umenena
 
Mtatiro na uhakika angeweza kuwa mbunge lakini walimpandikiza akagawe kura za Upinza ubungo, Sisi tunalifahamu hili kwa undani kwa sababu Mtatiro alikuwa anamuunga JJ Mnyika toka 2005 tuko naye Chuo sasa iweje leo anakuja kumpinga kwa kutumia kauli mbiu za CDM kama Peoples Power, 2010 Hatudanganyiki etc.

Huyu jamaa mimi sina imani naye maana angegombea hata temeke au kwingine angepata kura nyingi.

Najua hata watu wa CUF hili hawakulifahamu kwamba kupandikizwa kugawa kura za upinzani kunaweza kukufanya ushindwe kabisa.

Peoples Power
 
Duh! kuibadilisha hiyo ya CUF kuwa si watu wa vibaraghashia ni kazi ambayo imeshindikana kabla ya kuianza....Jaribu lakini na ujue mgovi wako hapo ni yule wa 1995 aliyekuonyeshea na visu vyako kabisa...usije pambana na CDM wao wasikilizaji ktk hili sema na mapambio kidogo huwa wanaaitikia vibwagizo
 
Angetuthibitishia kwanza kama huo unaibu mkuu amepewa ili kuonyesha umma wa Watanzania kwamba CUF si chama cha kidini.
 
Unaendelea kunifata fata tu! MODs remove this GAY from the forum

Mh!siamini kama unamaanisha GAY,au umeteleza tu,lengo lako lilikuwa kumuita GUY.Can please defferenciate these words!!to the best of my knowledge GAY means indicating, or supporting homosexual interests.on the other hand GUY means persons of either sex; people.
 
Mimi nadhani Mtatiro amepotea njia, nimeisoma ile makala nikamwona kuwa kwenda kwake CUF nikukengeuka tu. Na nataka nimuhakikishie kuwa CUF ni chama kigumu sana kutokana na misingi yake ya awali na ndiyo maana kinakosa nguvu huku bara. Ni chama chenye asili yake Pemba sasa unategemea nini? Mtatiro toka huko wewe ni kijana shupavu, na mimi nilitamani uwe bungeni lakini nilijua hutafika kupitia CUF kwani hicho ni cha wapemba no wonder ni mbunge mmoja tu bara aliyepatikana kwenye ballot, wengine wote ni wapemba ambao wameingizwa bungeni kutokana na katiba mbovu tuliyo nayo.
 
Hiyo dhana haiwezi toka ,mfano we angalia cuf kipo hasa maeneo gani? Ni maenel ambayo ni waisalamu wengi kwa bara ni ukanda wa pwani tanga ,kilwa,lindi,zanzabar

same apply to CDM kinaumaarufu au kupendwa ukanda wenye wakristo wengi kilimanjaro, mwanza, mbeya, iringa etc etc
 
Yep, tuna matatizo ya mtazamo wa kidini katika vyama vyetu hivyo juhudi za kuufuta zinakaribishwa sana. Lakini hilo litawezekana tu kwa kila chama kufanya kazi nzito ya kisiasa kutanua ufuasi kwa kukieneza sehemu zote na kuhakikisha nafasi za uongozi zinapata watu makini toka dini zote na makabila yote.

Hata hivyo, tatizo kubwa la CUF hivi sasa ni kuonekana kama chama cha visiwani tu. (CDM nao bado hawajapenya huko). Pia ndoa ya CUF na CCM huko visiwani lazima italeta changamoto kubwa sana kwa CUF kujiimarisha kama chama cha upinzani. Pamoja na kazi ya kisiasa kueneza vyama, kwa upande mwingine, mambo haya yanamalizwa na kukua kwa elimu ya kweli katika jamii jambo ambalo serikali ya sasa ina utashi wa kuliminya kisawasawa na kuendeleza kampeni za kupotosha umma (udini, ubaguzi wa rangi, n.k.).

Kwa upande wa CCM (ambao bila shaka wanaikodolea macho thread hii kama kunguru ashuhudiavyo malumbano ya panzi akisubiri vita ianze!) wao wana nyenzo kuu mbili. Kwanza ni kuwa madarakani; pili, ni kurutubisha mfumo wa ufisadi. Hapo asikwambie mtu, hakuna cha dini, rangi, kabila wala ukoo; mafisi, ma-nzi, madumuzi, mchwa, wote wanajumuika na kamwe hawaulizani: yakhe, wasali wapi au watokea pande ipi vile? Wala vibarghashia na misalaba haiwapi tabu kabisa. Kinachoangaliwa ni mtiririko wa ulaji tu. Wapinzani au wanaharakati wakiwasumbua, wanawatupia fupa la udini, ukabila, n.k. wahangaike nalo.
 
dhana ya dini ni ya CCM ukweli ni kuwa CHADEMA ni bara na CUF ni zanzibar tuu.. tusubiri katiba mpya my tanganyika ipewe hadhi kuliko kudharauliwa kama zamani..... Basi CHADEMA tunakula nchi kama tunanawa na mafisadi wooote tunawafunga,, tunabaki CHADEMA na wananchi tuu kuyapiga maziwa na asali za nchi hii... Elimu bure mpaka Phd NGUVU YAKO TUUU.... Kila mwekezaji lazima ugawe kipato wa wakazi wa karibu hapo tuu.. Sheria ya fisadi anyongwe kama China vile... Akii ya nani tutawaacha akina Maalim wakifisid Zanzibar kama alivyozoea na wenzake akina Rashid tuliowatenga kwa kuwa budget ya upinzani na matumizi hata hapakuwa na statement ya matumizi... aliiba saaana... hizo mil 200 kila mwezi za upinzani tutatumia kwa operesheni tuu hakuna kulala... waacheni CUF waendelee na ufisadi wao 20005-2010 walikuwa wakipata mill 99 pamoja na 200mil za kambi ya upinzani lakini wapi???? CHADEMA mwisho wa siku ikang'ara kwa kuwa pale hakuna udini au kusilimu ni kazi tuuu... ukianza kupenda kuwa tajiri kama Zitto kwa kuvuruga chama tunakutimua tuuu
Hizi hesabu za kichina zimenipiga chenga mkuu wangu. Naomba kuwasilisha. -😉
 
Mtatiro na uhakika angeweza kuwa mbunge lakini walimpandikiza akagawe kura za Upinza ubungo, Sisi tunalifahamu hili kwa undani kwa sababu Mtatiro alikuwa anamuunga JJ Mnyika toka 2005 tuko naye Chuo sasa iweje leo anakuja kumpinga kwa kutumia kauli mbiu za CDM kama Peoples Power, 2010 Hatudanganyiki etc.

Huyu jamaa mimi sina imani naye maana angegombea hata temeke au kwingine angepata kura nyingi.

Najua hata watu wa CUF hili hawakulifahamu kwamba kupandikizwa kugawa kura za upinzani kunaweza kukufanya ushindwe kabisa.

Peoples Power
Una maana kwa hiyo CUF wanampa tuzo (reward) kwa kazi nzuri aliyoifanya kugawa kura za wapinzani ingawa hawakufanikiwa siyo? Angalau alikuwa royal to his masters
 
Hivi ni nini kilichotokea mpaka Mzee Bernard Mapalala kuondoka CUF ili hali yeye ni Founder or Co-Founder?
 
Back
Top Bottom