kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,126
- 24,419
Kiongozi wa Upinzani Afrika Kusini asema Kenya ni koloni la Marekani, akipigia chapuo Kiswahili
Kiongozi maarufu wa upinzani nchini Afrika Kusini amekosoa vikali safari ya hivi karibuni ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya nchini Marekani na mazungumzo yake na rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
Julius Sello Malema, ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF), ameongeza kuwa, Kenya ni koloni la Marekani na kwamba hakuna 'uhuru kamili' katika nchi hiyo kwani Marekani inadhibiti mambo mengi yanayojiri Kenya.
Aidha amesema kuna haja kwa nchi za bara la Afrika kujikwamua kutoka katika tatizo hilo la ukoloni mamboleo.
Mapema mwaka huu Trump alizitukana nchi za Afrika kuwa ni 'shimo la kinyesi' jambo ambalo lilikosolewa vikali na viongozi wa Afrika.
Kwingineko Malema amependekeza bara la Afrika liungane na liwe na sarafu yake moja kama ilivyo kwa nchi za Ulaya na kutumia lugha moja ya Kiswahili ili kuepuka lugha za kikoloni ambazo zinatumiwa kututenganisha.
Malema aliyasema hayo Agosti 29, 2018 kwenye mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na chama chake cha EFF kama sherehe ya miaka mitano tangu chama hicho kianzishwe. Aidha alizungumza kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ujumbe wa Rais wa Marekani kwenye mtandao wa Twitter kuhusu marekebisho ya sheria ya ardhi Afrika Kusini ambapo amesema bara la Afrika haliwezi kukubaliana na Trump ambaye anawatetea Wazungu makaburu waliopora ardhi za Waafrika wazalendo
Sent using Jamii Forums mobile app