Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,267
Mgombea wa nafasi ya makamu wa urais katika klabu ya Simba amesema anaidai klabu hiyo zaidi ya Sh. milioni 200.
Jamhuri Kihwelo ‘Julio' amesema anadai kitita hicho kilichotokana na kuvunja mkataba wakati akiwa kocha, lakini madai ya mishahara na marupurupu yake.
Tokea enzi za uongozi wa (Hassan) Dalali, Simba ina fedha zangu na hadi leo hawajanilipa. Zaidi ya Shilingi milioni mia mbili, nawadai na hata mzee Dalali analijua hilo, hivyo ninataka kulipwa.
Wasipofanya hivyo sitakuwa na msamaha, nitawapeleka mahakamani, alisema Julio. Julio amechukua fomu za ugombea nafasi ya makamu na kufanikiwa kurejesha kwa wakati mwafaka.
Sasa atapambana na Swedi Nkwabi pamoja na Geofrey Nyange ‘Kaburu'.