Mtela Mwampamba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 537
- 347
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WABUNGE WAONESHE UZALENDO KWA KUCHANGIA UNUNUZI WA MADAWATI, KULAANI JESHI LA POLISI DODOMA
Ndugu wanahabari;
Tumewaita hapa kwa nia ya kuwaomba mtufikishie hoja zetu mbili juu ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwataka waoneshe uzalendo kwa kuchangia kampeni ya ununuzi wa madawati na pia kizalendo kabisa kulaani Polisi Dodoma kuwatawanya wanafunzi waliokuwa katika mahafali yao ya ngazi ya Chama.
Suala la wabunge
Mtakumbuka kuwa hivi sasa wadau mbalimbali nchini wanaendelea kuungana na watendaji wa Serikali kuunga mkono agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati.
Hata hivyo pamoja na jitihada za mbunge mmoja mmoja katika ngazi ya jimbo lake kwa baadhi ya wabunge, kwa ujumla wawakilishi hao wa wananchi wengi wao hawaonekani kuunga mkono juhudi hizi katika ngazi ya kitaifa.
Jukwaa linasikitishwa na hali hii na linawasihi wabunge badala ya kuegama zaidi katika masuala ya siasa, kuungana na wadau wengine nchini kumuunga mkono Rais kwa kusamehe sehemu ya posho yao ya vikao ili zichangie madawati nchi nzima.
Tunafahamu kwamba Bunge letu lina takribani wabunge 383 ambao wanalipwa posho za aina mbili; posho ya kikao (Sitting allowance) ya Sh. 220,000 na posho ya kujikimu (Per-diem) ya Sh. 120,000 kwa siku.
Sisi tukiwa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania tunaomba wabunge wetu waunge mkono jitihada za Mh. Rais kwa kuchangia posho yao ya kukaa kitako yaani Sitting allowance ya siku 10 zilizobaki za Bunge.
Iwapo watafanya uamuzi wa kizalendo kwa siku 10 tu watakuwa wamechangia Sh. 842,600,000 na kwa gharama za dawati moja ni wastani wa sh 60,000, kwa hiyo watakuwa wamechangia jumla ya madawati 14,043 ambayo yatasambazwa nchi nzima hasa katika mikoa yenye uhitaji zaidi.
Jukwaa linaona sababu zifuatazo kwa wabunge kuchukua hatua hiyo ya kizalendo ambazo ni:
(1)Kuunga mkono kauli na dhamira ya Mh.Rais Magufuli.
(2)Kuwaunga mkono wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wameunga mkono agizo la Mh.Rais kwa vitendo kwa mfano Taasisi za Dini,Taasisi za Fedha,Wafanyabiashara,Wasanii,Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Tanzania,Mafundi Gereji na wengineo
(3)Kuwatia moyo,motisha na ushawishi kwa wadau wengine ambao hawajajitokeza bado maana Wabunge ni kioo cha jamii.
(4)Ni kitendo cha kizalendo katika jamii inayowazungunga.
(5) Wabunge wetu pia watakuwa wanatilia nguvu hoja mpya ya kuwa na Tanzania yenye hamasa ya kuchangia zaidi shughuli za maendeleo badala ya watu kuchangia zaidi vitu kama harusi na siasa tu.
Tunawaomba wananchi wa majimbo mbalimbali wafuatilie kwa karibu na kuwawajibisha kisiasa wabunge wao ambao hawatakuwa mstari wa mbele katika kuchangia madawati na shughuli nyingine za kijamii na kitaifa.
Kulaani Polisi Dodoma
Mwisho Jukwaa linalaani kitendo cha Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kuzuia Mahafali ya Vijana wa Chadema (Chaso).
Jukwaa linaomba Serikali ifanye uchunguzi wa haraka na kubaini tatizo lilikuwa ni nini mpaka kutumia nguvu ya Dola kiasi kikubwa pasipo na ulazima kwa wanafunzi wale.
Kwani kitendo kilichofanyika kinajenga chuki,uhasama na ubaguzi kwa baadhi ya vijana wanaounga mkono vyama vyao na pia inaleta chuki kati ya Serikali na WanaNchi.
Jukwaa linaomba haki itendeke kwa vijana wote wanaounga mkono vyama vyao vya siasa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.Lakini pia Tunaomba WanaNchi wafuate kanuni,taratibu,sheria na katiba za nchi kwa kila jambo na shughuli wanazozifanya maana nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na Katiba.
Tunawashukuru kwa kutusikiliza.
Imetolewa:
Jumapili 19/06/2016 Mkoani Iringa
Katibu wa Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania.Mtela Mwampamba:0755178927