Juisi ya kitunguu: Huponya yaliyoshindikana hospitali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Juisi ya kitunguu: Huponya yaliyoshindikana hospitali!

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Juisikitunguuu.jpg

  Katika makala ya leo nawaeleza faida za juisi ya kitunguu maji katika mwili wako, ikiwemo uwezo wake wa kuzuia na kutibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana kwa kutumia dawa za hospitali.


  Tunapaswa kutambua kwamba viungo vingi tunavyotumia jikoni kwenye vyakula vyetu kila siku vina uwezo mkubwa wa kuponya magonjwa yanayotusumbua. Sina shaka kama kuna mtu ambaye hakijui kitunguu, nyanya, au kitunguu saumu.


  Kitunguu maji ni kiungo cha mboga, ambacho aghalabu hutumika katika mapishi ili kuongeza ladha katika chakula na wakati mwingine hutumika kutengenezea kachumbari. Baadhi ya watu hawapendi kula kachumbari kwa kutokujua umuhimu wake mwilini.


  KITUNGUU KINATIBU YAFUATAYO

  Katika orodha ndefu ya magonjwa yanayotibika PASIPO SHAKA kwa kutumia juisi ya kitunguu, ni pamoja na ugonjwa unaowasumbua watu wengi wa kutokwa na damu sehemu ya haja kubwa wakati wa kujisadidia.


  Ugonjwa huu, ambao kwa kitaalamu unajulikana kama ‘hemorrhoids' au ‘Piles', unawatokea watu wengi ambao kama mtu hukupata nafuu kwa kula vidonge, suluhisho la mwisho huwa ni kufanyiwa upasuaji mdogo katika njia ya haja kubwa, upasuaji ambao huambatana na maumivu makali.


  Kwa wale ambao wameshakutwa na tatizo hili au wanalo hadi sasa, dawa kama vile ANUL SUPPOSITORIES, SECNIDAZOLE, n.k zinajulikana sana kwao, kwa sababu ndiyo dawa zinazopendekezwa na madaktari wengi kutumiwa ili kutibu PILES. Unaweza ukapona kwa muda na tatizo likajirudia baadaye au unaweza usipone na ukalazimika kufanyiwa upasuaji.


  Lakini kwa kutumia juisi ya kitunguu, unaweza ukapona kabisa na inawezekana tatizo lisijirudie, kwani mzizi wa tatizo huondoka kabisa kutoka tumboni.


  SIFA YA KITUNGUU

  Kitunguu kina virutubisho vyenye uwezo wa kuua bakteria (antibacterial) na fangasi mwilini. (anti fungus). Pia kina virutubisho vyenye uwezo wa kuzuia wadudu wanaosababisha magonjwa nyemelezi (anti free radicals) na magonjwa ya uvimbe (anti informatory).


  Mbali na sifa hizo, kitunguu kina kiwango kikubwa cha madini kama vile ‘calcium', ‘magnesium', ‘sodium', ‘potassium', ‘selenium', ‘phosphorus' na bila kusahauu kiasi kidogo cha aina fulani ya mafuta ambayo huimarisha kinga ya mwili.

  JINSI YA KUJITIBU ‘HEMORRHOIDS.'


  Kama nilivyoanza kusema awali, pamoja na magonjwa mengine yanayotibika kwa kitunguu, leo tutaanza kwanza na ugonjwa huu unaosumbua watu wengi. Dawa hii ni ya uhakika kwa mtu atakayeweza kuitumia kama inavyotakiwa.


  Kunywa juisi ya kitunguu kila siku asubuhi kwa muda wa siku saba hadi siku 14, ikitegemea na ukubwa wa tatizo lako. Juisi hiyo lazima uinywe asubuhi kabla ya kula kitu chochote (on empty stomach) na utaruhusiwa kunywa kifungua kinywa chako saa moja baada ya kunywa juisi hiyo.


  Dozi hii ni maalum kwa ajili ya kutibu ‘hemorrhoids', ingawa wakati ukitibu tatizo hilo, matatizo mengine yaliyomo mwilini yatakuwa yakijiondoa, kama tutakavyoona katika makala haya wiki ijayo. Napenda kukuhakikishia kuwa tiba hii ni ya uhakika na haina madhara yoyote.


  TAHADHARI

  Mara baada ya kuinywa juisi hii kwa mara ya kwanza na siku chache zitakazofuata, utajisikia vibaya na tumbo kuchafuka. Hali hii ni ya kawaida, unachotakiwa kufanya mara baada ya kunywa, ni kukaa au kulala kwa muda, baada ya muda hali yako itarejea kama kawaida. Baada ya siku tatu, ukinywa mwili utaizoea na utajisikia kawaida tu.
  ​JUISI YA KITUNGUU: HUPONYA YALIYOSHINDIKANA HOSPITALI! - Global Publishers

   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  kitunguuu.jpg


  Wiki iliyopita tulianza makala haya kwa kuangalia jinsi kitunguu kinavyoweza kutibu ugonjwa wa kutokwa damu wakati wa kutoa haja kubwa. Katika makala hayo, watu wengi wameonekana kuguswa nayo. Wiki hii, pamoja na mambo mengine, nitakujuza jinsi ya kuitengeneza juisi hiyo.

  Halikadhalika katika makala ya leo, utajua magonjwa mengine yanayoweza kutibika kwa kitunguu, iwe kwa kunywa juisi yake au kwa kula kitunguu chenyewe. Kitu kimoja napenda kukuhakikishia kuwa, unayoyasoma hapa kuhusu kitunguu, tayari yalishafanyiwa utatifi na kuthibitishwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya vyakula tangu enzi za mababu zetu.

  Vile vile, watu wanaoamini lishe kama tiba na kutumia, matokeo yake siku zote huwa dhahiri na wako wengi wanaoweza kuthibitisha jinsi afya zao zilivyo imara leo tofauti na miaka kadhaa iliyopita kabla ya kugundua siri ya chakula kama tiba.

  JINSI YA KUTENGENEZA
  Kinachotakiwa ni kitunguu maji kimoja cha ukubwa wa wastani ambacho utatengenezea juisi na kupata kiasi cha glasi moja saizi ya kati. Safisha kitunguu chako kwa kuondoa gamba la juu kisha katakata vipande vidogo vidogo ili kurahisisha usagaji.

  Kuna njia mbili unazoweza kuzitumia kutengeneza juisi hiyo. Ya kwanza ni ya kisasa ambapo unaweza kutumia ‘blender' au ‘juicer', kwa kuweka maji kidogo na kuanza kuisaga hadi kupata juisi. Njia ya pili ni ya kiasili, ambapo utatumia kinu kidogo na maji kidogo kwa kutwangwa hadi kupata juisi.

  Ukimaliza kusaga (kwa njia utakayoitumia) kamua na ichuje juisi yako kwa kutumia chujio la kawaida ili kupata juisi pekee ya kitunguu na kuacha masalia ya maganda peke yake. Mara baada ya kuiweka juisi yako kwenye glasi, HAKIKISHA UNAINYWA HAPO HAPO. Hairuhusiwi kuihifadhi au kuinywa baadaye, kwa sababu itapoteza virutubisho vyake muhimu.

  Kunywa glasi moja mara moja kwa siku au mara mbili, ukiona tatizo lako ni kubwa. Fanya zoezi hilo la kundaa juisi na kuinywa kwa muda wa siku saba hadi 14.
  Kama nilivyoeleza wiki jana, hali ya kuchafuka kwa tumbo na kujisikia vibaya baada ya kunywa, isikuogopeshe, baadaye utaizoea na utajisikia vizuri zaidi.

  Mbali ya kutibu tatizo la kusikia maumivu na kutokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa (Hemorrhoids au piles), juisi hiyo pia itatoa ahueni au kinga kubwa dhidi ya matatizo mengine ya kiafya yafuatayo:
  Pumu, mafua, magonjwa ya kuambukizwa na bakteria, matatizo ya kupumua kwa shida, kiungulia na kutapika.

  Itaongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi, vile vile kwa kutafuna vitunguu vibichi na kukaanavyo mdomoni kwa sekunde kadhaa, kutaua bakteria wote wa kinywani na kutoa kinga dhidi ya kuoza kwa meno na kuondoa harufu mbaya.

  Ulaji wa vitunguu maji vibichi mara kwa mara, hulainisha damu na kuzuia kuganda ambako husababisha mishipa kuziba na kusababisha magonjwa ya moyo, ikiwemo presha ya kupanda.

  Juisi ya kitunguu ni dawa mara moja ya kuzuia kutapika, mtu anayetapika mfululizo akinywa juisi ya kitunguu, hupata nafuu haraka. Vile vile juisi hii ni dawa ya tumbo linalouma na hutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe tumboni.

  Kama unasumbuliwa na chunusi, pakaa juisi ya kitunguu iliyochanganywa na asali sehemu yenye chunusi vitaondoka na kukuacha na ngozi nyororo. Chukua kiasi kidogo cha juisi na kijiko kimoja kidogo cha asali changanya kisha pakaa.

  Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya kutibu majeraha ya kuumwa na nyuki. Kama unapata maumivu wakati wa haja ndogo au unatoa mkojo mchafu sana, kunywa maji mengi yaliyochanganywa na juisi ya kitunguu kiasi kidogo, tatizo litakwisha.

  Juisi ya kitunguu ina virutubisho vyenye uwezo wa kudhibiti chembechembe hai za mwili zenye kansa na hivyo kuwa kinga nzuri dhidi ya ugonjwa wa saratani (cancer).

  Ulaji wa vitunguu au juisi pia hutoa ahueni kwa mgonjwa wa kifua kikuu. Juisi iliyopashwa moto pia ni dawa ya sikio linalouma. Weka matone mawili tu kwa kila sikio linalouma.

  Juisi ya kitunguu pia ni dawa ya majeraha yatokanayo na moto. Ukiungua, pakaa juisi hiyo sehemu zilozoungua kwa nafuu ya haraka. Pia kitunguu ni dawa ya mbu, pondaponda vitunguu, kisha jipakae sehemu za miguu na mikono - mbu hawatakugusa.

  Faida za kitunguu na juisi yake ziko nyingi na zote ni muhimu kwa ustawi wa afya zetu. Nakushauri kuanzia leo, kunywa juisi hiyo au kula kitunguu katika kila mlo kwa jili ya kutibu maradhi uliyonayo au kwa kuupa mwili wako kinga imara, na kamwe hutajuta!


   
 3. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante sana kaka kwa somo.
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Swali langu ni kwamba baada ua kutumia hiyo juisi utumie nini ili kukata harufu ya vitunguu mdomoni. sababu wakati miwingine haipendezi.
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mzizimkavu tunashukru sana kwa shule ya afya
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu@Mwanaweja Karibu unakaribishwa sana Kwenye jukwaa letu tukufu la afya.
   
 7. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mimi Nina wasiwasi Na testi. Kitunguu maji, juisi du, kwanini mtu asikile hivihivi Na chumvi ni maramia kuliko juisi.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu@Remmy ndio maana ikaitwa dawa, dawa hata kama ikiwa ni chungu sana ili mradi itibu tu yale maradhi uliyokuwa nayo ndipo inapofaa na kuitwa dawa haihitaji iwe na ladha nzuri dawa inahitaji ifanye kazi yake ya kidawa Mkuu.upo na mimi.?
   
 9. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mzizimkavu mm huwa natumia vitunguu swaumu kwa kutafnia na slice za mikate. hii imekaaje mkuu maana bibi yangu alikua anashauri kutumia vitunguu swaumu kwa kua ni dawa ya maradhi mbalimbali. Sasa mkuu hapa unashaurije?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  @Petiro Ni Vizuri ila ukimaliza kula itabidi uwe unakula japo kipande cha Karoti au kipande cha tangawizi kukata harufu ya kitunguu mdomoni maana unavyofanya wewe ukiwa karibu na rafiki yako au mpenzi wako ukizungumza basi utatowa harufu ya kitunguu saumu. Jaribu kufanya hivyo ili harufu ya kitunguu saumu ikatike.
   
 11. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  kuwa scientific kidogo mkuu: glass ya saizi ya kati (= mls ngapi?) , kitunguu cha saizi ya wastani (= gram ngapi?) , weka maji kidogo (= mls ngapi?) . Maana nataka nitumie kiasi kile chenyewe ili baadae( baada ya siku 14) nikupe feedback.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  How to Make Garlic Juice?

  Instead of buying garlic juice from the grocery stores, a better option is to make it on your own. All you need is some spare time and some fresh cloves. Needless to say, garlic juice recipe requires preparing the cloves first. Remember that hundreds of cloves are used for making a few ounces of garlic juice. Accordingly, peel garlic cloves as per your required juice amount. Make use of a plastic garlic peeler for quick peeling of the cloves. The next step is making a puree out of the garlic cloves.

  Add peeled garlic cloves in a food processor and blend till you get a puree. Or, you can crush garlic directly by using a garlic press. Then, place a muslin cloth over a small bowl and strain garlic puree. Press the pulp with a small spatula to collect maximum juice. If you want a pure juice without any pulp, consider filtering again with the help of a coffee strainer. Once you are done with the straining part, transfer garlic juice in a glass container and store in the refrigerator.

  This is how you can make homemade garlic juice. Spraying on some garlic juice converts a plain tasting salad or dish into a flavorful one. No wonder, it is highly appreciated by people on low-calorie diet and low-sodium diet. Speaking about garlic juice substitute, you can replace ½ teaspoon of garlic juice with 1 teaspoon chopped garlic or ½ teaspoon minced garlic. If you have garlic powder, then also you can add ⅛ teaspoon garlic powder in substitution for ½ teaspoon garlic juice.
   
 13. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mzizi bado nasubiri majibu ya maswali yangu!
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  @Rubi nimekujibu soma chini

  @Rubi Dawa ya Kutowa Harufu mbaya mdomoni ya kitunguu saumu ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa Maziwa au kunywa maji mengi. Au Tumia Tangawizi mbichi tafuna baada kula kitunguusaumu pia inaondosha harufu mbaya ya mdomo, Unaweza pia kutafuna karafuu baada ya kula kitunguusaumu pia karafuu inakata harufu ya mdomo.

  Na harufu ya kitunguu maji huondoshwa kwa kula Nanaa kwa kiingereza inaitwa (Mint).
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Did You Know?

  Onions contain chemicals which help fight the free radicals in our bodies. Free radicals cause disease and destruction to cells which are linked to at least 60 diseases.

  When a person eats at least 1/2 a raw onion a day, their good type HDL cholesterol goes up an average of 30%. Onions increase circulation, lower blood pressure, and prevent blood clotting.
   
 16. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,170
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  siku moko kuna dada alinirecomend ninywejuice ya nyanya ni poa. Nikamwambia jaza glass dada. Mbona nilijuta! Pa kuimwaga ile juice sioni. Nikafumba macho, nikapiga mkupuo moko. Sirudii tena.
  Sasa vitunguu, duh! will c if i can try as little as a sip
   
Loading...