Kitaalamu sukari hasa ya viwandani ni kitu kisicho na virutubisho vyovyote kwa binadamu. Kazi yake kubwa ni kukufanya upate ladha ya utamu tu.
Hivi juice ya miwa haiwezi kutumika kama mbadala wa sukari kama vile asali inavyutumika? Kwa mfano ukikoroga uji au chai unaweka kiwango fulani cha juice ya miwa, ukipika maandazi unatumia juice ya miwa kukandia unga n.k
Lakini pia watu wazima wanaweza kujifunza kutotumia sukari ya viwandani ya kuongeza katika chai, kahawa
Kama watu wazima nchi hii wangeweza kuachana na sukari ya viwandani tungeokoa mamilioni ya dola na pia kupunguza matumizi.
Naona hata kampuni za bia na juice siku hizi wanajivuniza kutoongeza sukari katika nyingi ya bidhaa zao.