Unafanyaje kuimarisha kinga ya mwili kipindi hiki cha mlipuko wa COVID-19?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
126
500
Ugonjwa wa Corona Virus (COVID-19) huathiri zaidi wale ambao kinga yao ya mwili iko chini kama wazee, wajawazito na wale wenye hali nyingine za kiafya kama magonjwa ya pumu na mengine ya mfumo wa upumuaji.

Tumekuwa tukipeana mbinu za kujikinga na ugonjwa kama kunawa, kutoshika uso, kukaa ndani na kadhalika. Pia tumekuwa tukielekezana vya kufanya endapo tutapata kama kujitenga na kadhalika.

Je, tujiandae vipi endapo itatokea kwa bahati mbaya tumepata maambukizi?
Hizi ni njia 6 za kuboresha kinga ya mwili ili kupunguza athari za virusi hivyo

1. Punguza msongo wa mawazo
Unapokuwa na msongo wa mawazo, mwili hutengeneza vichocheo ambavyo hupunguza kinga ya mwili. (Ushawahi kujisikia kuumwa unafika kwa daktari akakwambia ni stress tu hizo?)

Corona inatisha lakini jitahidi kupunguza msongo na kuwa na mawazo chanya kwa kufanya vitu vinavyokufurahisha.

2. Lala uchokapo
Usingizi ni njia ya mwili kujiweka sawa. Unapokosa usingizi unaumiza mfumo wako wa kinga. Lala kadri mwili wako unavyohitaji.

3. Tumia vyakula vyenye kuimarisha kinga
Machungwa, Vitunguu saumu, Brokoli na Spinachi ni mifano ya vyakula hivi. Vitumie kwa wingi.

Kama unahisi mfumo wako wa kinga uko chini, unaweza kutumia vijazilizi vya vitamini kama Vitamini C, Vitamini B, Vitamini D, and Zinc.

4. Punguza “Inflammation”
Inflammation ni kitendo cha sehemu ya viungo vya mwili kuvimba, kuwa nyekundu huku mara nyingi ikiambatana na maumivu.

Sukari, nyama zilizosindikwa, mafuta ya mimea na pombe husababisha hali hii na kuupa kazi mfumo wa kinga ya mwili na kuufanya usiweze kupambana na matatizo mengine kwa ufasaha.

5. Fanya mazoezi ya wastani
Mazoezi ni moja ya mambo bora ya kufanya ili kuboresha kinga ya mwili lakini umakini unahitajika ili kutouchosha sana mwili na kuleta athari hasi kwa kinga ya mwili.

6. Epuka sumu mbalimbali
Kuna vitu kadhaa tunavyokutana navyo kila siku ambavyo vina sumu. Hivi ni vya kuepuka hususani wakati huu ambapo tunaihitaji kinga ya miili yetu kuwa ngangari.

Vitu hivi ni kama dawa za kuua vijidudu kwenye mimea, maji ya kunywa yenye klorini, sumu mbalimbali za kwenye hewa kama moshi wa viwandani na kemikali za kuongeza ladha au rangi kwenye chakula.

PIA SOMA
View attachment 1419501

ULAJI wa mlo kamili zikiwemo mbogamboga, matunda na maji kwa wingi, imelezwa kuwa ni miongoni mwa virutubisho vinavyoongeza kinga ya mwili katika kupambana na virusi vya corona. Aidha, imetolewa angalizo kwa jamii kuepuka upotoshaji unaoenezwa kwamba kujifukiza ni moja ya tiba ya virusi vya corona, akisema njia hiyo sio sahihi kwa sababu inaweza kuleta athari ya kuunguza njia ya hewa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa Programu wa Elimu ya Afya kwa Umma katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Tumaini Haonga amesema mlo kamili na unywaji maji kwa wingi, vinasaidia kujenga kinga imara zitakazoweza kukabiliana na virusi hivyo, vinavyosababisha homa kali ya mapafu (Covid-19). “Katika kipindi hiki cha mlipuko ni muhimu kuzingatia lishe sahihi yaani ulaji wa chakula ambacho ni mlo kamili.

Mtu mwenye hali nzuri ya lishe ana uwezekano mkubwa wa kuwa na kinga imara ya mwili na hivyo mwili wake utaweza kupambana na vimelea vya magonjwa ikiwemo virusi vya corona kwa kiwango kikubwa zaidi ukilinganisha na wengine,” alisema Dk Haonga. Alisema mlo kamili ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu ikiwemo wanga, protini, mafuta kiasi, madini joto, vitamini, mbogamboga na maji ya kutosha mara kwa mara. “Tunapoangalia mlo kamili tuangalie mchanganyiko wa vyakula kulingana na upatikanaji na uwezo wa mtu kuendelea kuvipata, mboga za majani aina zote, matunda na maji kwa wingi ni muhimu sana katika kipindi hiki,” alifafanua daktari huyo.

Dk Haonga alisema ulaji wa kiwango cha juu cha virutubishi fulani, huimarisha mfumo wa kinga, huku ulaji wa kiwango cha chini ukidhoofisha kinga na kuvutia maradhi ya maambukizi. “Kinga imara mwilini inaweza kusaidia kukabiliana na virusi, na pia inaweza kuwasaidia baadhi ya wagonjwa kupona kwa haraka,” alisisitiza. Alitaja virutubisho vinavyoweza kuimarisha kinga ya mwilini ni kama vile madini ya zinki, iron na vitamin A, C, D, E, B-6, vyakula kama vile kabichi, broccoli, mchicha, chai ya kijani, samaki, maharage, uyoga, viazi vitamu na matunda kama tufaa, mananasi, maembe na machungwa, machenza na mengineo.

Alisema vyakula hivyo ni muhimu katika kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya milipuko. Baadhi ya madaktari walisema matunda kama vile machungwa, yana vitamin C nyingi ambayo ina uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Pia virutubisho hivyo vinasaidia kuzuia uvimbe kupitia kiasi na uharibifu wa tishu, unaosababishwa na virusi hivyo, ambao unaweza kusababisha majeraha ya mapafu na hata kifo. Aidha, Dk Haonga alisema vyakula hivyo vinaweza kuwa muhimu kwa watu wazima, ambao wako hatarini zaidi kuambukizwa maradhi ya Covid-19.

Alisema uzoefu kutokana na milipuko mingine ya magonjwa ya maambukizi, unaonesha wazi kwamba watu wanaokula lishe duni wako hatarini zaidi kuambukizwa virusi hivi. Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya hadi juzi mambukizi mapya ni 17, waliopona na kuruhusiwa ni saba, vifo vitatu hivyo kufanya mambukizi kufikia 49. Pia takwimu hizo zinaonesha wanaofuatiliwa kubaini kama wameambukizwa au la ni 590, waliomaliza ufuatiliaji ni 413 na wasafiri waliopo kwenye karantini ni 84. Maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa nchini ni Dar es Salaam (wagonjwa 32), Zanzibar (12), Arusha (3), Kagera (1) na Mwanza (1).
 

Kiziwanda chema

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
261
500
Vitu hivi ni kama dawa za kuua vijidudu kwenye mimea, maji ya kunywa yenye klorini, sumu mbalimbali za kwenye hewa kama moshi wa viwandani na kemikali za kuongeza ladha au rangi kwenye chakula.
Tobaa... Dawasco Siku hizi wanajaza Chlorine ya kutosha kwenye Maji ya bomba hadi unasikia uchungu ukiyanywa maji. Wallahi watatuua Wapunguze Kwakweli
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,211
2,000
4. Punguza “Inflammation”
Inflammation ni kitendo cha sehemu ya viungo vya mwili kuvimba, kuwa nyekundu huku mara nyingi ikiambatana na maumivu.
Mkuu boresha kidogo maana halisi ya inflammation.
Hiyo uliyoweka ni sehemu mojawapo tu ya athari za inflammation lakini sio tafsiri au maana ya inflammation..

Athari zingine inaweza kuwa joto kali, homa kali, kushindwa kufanya kazi sehemu flani ya mwili, maumivu, uchovu, kutokwa vipele vidogo (rashes), maumivu ya viungo, kutokwa vidonda mdomoni, kuvimba tezi, n.k.

Inflammation is a defense mechanism in the body. The immune system recognizes damaged cells, irritants, and pathogens, and it begins the healing process.

When something harmful or irritating affects a part of our body, there is a biological response to try to remove it. The signs and symptoms of inflammation can be uncomfortable but are a show that the body is trying to heal itself.

Symptoms of inflammation vary depending on whether the reaction is acute or chronic.

The effects of acute inflammation can be summed up by the acronym PRISH. They include:

 • Pain: The inflamed area is likely to be painful, especially during and after touching. Chemicals that stimulate nerve endings are released, making the area more sensitive.
 • Redness: This occurs because the capillaries in the area are filled with more blood than usual.
 • Immobility: There may be some loss of function in the region of the inflammation.
 • Swelling: This is caused by a buildup of fluid.
 • Heat: More blood flows to the affected area, and this makes it feel warm to the touch.
These five acute inflammation signs only apply to inflammations of the skin. If inflammation occurs deep inside the body, such as in an internal organ, only some of the signs may be noticeable.

For example, some internal organs may not have sensory nerve endings nearby, so there will be no pain, such as in certain types of lung inflammation.

Symptoms of chronic inflammation present in a different way. These can include:
 • fatigue
 • mouth sores
 • chest pain
 • abdominal pain
 • fever
 • rash
 • joint pain
A person will notice inflammation symptoms after these steps take place.
Source: Inflammation: Causes, symptoms, and treatment
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom