JUA linawezaje kukosa kutua?”

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
Jambo hilo lenye kushangaza hutukia kwa sababu dunia inapozunguka jua kila mwaka, mhimili wa dunia huwa umeinama kwa digrii 23.5 kutoka kwa jua. Hivyo, wakati wa kiangazi katika Kizio cha Kaskazini, Ncha ya Kaskazini huinama kuelekea jua na wakati wa majira ya baridi kali ncha hiyo huinama mbali na jua. Kwa kuwa dunia huzunguka juu ya mhimili wake mara moja kwa siku, kwenye Mzingo wa Aktiki usikummoja kwa mwaka, yaani, karibu Juni 21, jua halitui. Vivyo hivyo, siku moja kwa mwaka, yaani, karibu Desemba 21, jua halichomozi, ingawa mchana huenda kukawa na nuru hafifu kama wakati wa mapambazuko.

Kwa kweli, kadiri unavyoelekea upande wa kaskazini juu ya Mzingo wa Aktiki, ndivyo jua linavyokosa kutua usiku wakati wa kiangazi na ndivyo jua hukosa kuchomoza siku nyingi wakati wa majira ya baridi kali. Kwenye ncha za Kaskazini na Kusini za dunia, kuna miezi sita ya mchana na miezi sita ya usiku.*

Watu wanaoishi kwenye ncha hizo za dunia hulalaje wakati wa kiangazi, nao hukabilianaje nasiku nyingi ambazo jua halichomozi wakati wa majira ya baridi kali? Zamani, katika jamii fulani, watu walilala saa maradufu katika miezi ambayo jua halikuchomoza kuliko walivyolala katikamiezi ambayo jua halikutua. Kuishi maisha ya kisasa kumewawezesha wengi kulala kwa muda uleule kila usiku. Lakini wakati wa kiangazi ambapo jua halitui, bado wakazi wa Kaskazini huwa na nguvu za ziada za kufanya kazi. “Inapokuwa mchana kabisa saa 5:00 usiku, sijisikii kwenda kulala,” asema Patrick, anayeishi Alaska. “Nyakati nyingine mimi hutoka na kwenda kukata nyasi au kufanya kazi nyingine.”

Kwa upande mwingine, miezi ambayo jua halitui au kuchomoza inaweza kuchosha kimwili nakisaikolojia. Hivyo, watu fulani hujaribu kuzuia nuru isipenye kwenye chumba chao cha kulala katika miezi ambayo jua halitui na kutumia taa wakati jua halichomozi, ili kusawazisha wakati wao wa kulala na kuzuia uchovu na kushuka moyo. Hata hivyo, licha ya magumu hayo, wakazina wageni wanakubali kwamba kushuhudia jua likiangaza katikati ya usiku ni jambo lisiloweza kusahaulika.
 
Back
Top Bottom