Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Nkurunziza amkubalia Magufuli sakata la Burundi
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, amekubali kushiriki mazungumzo ya kuleta amani nchini kwake baada ya kufanya mazungumzo na Rais Dk. John Magufuli hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa Ikulu jijini Dar es Salaam jana, ilimnukuu Waziri wa Mambo ya Nje Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Agustino Mahiga, akisema mazungumzo hayo yataongozwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na yatafanyika Desemba 28, mwaka huu nchini humo.
Mahiga aliyasema hayo mara baada ya Rais Magufuli kumaliza kukutana na mjumbe maalum wa Rais Nkurunziza, Spika wa Seneti, Reverien Ndikuriyo
“Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi mwishoni mwa wiki iliyopita ambaye amemhakikishia utayari wake wa kushiriki katika mazungumzo hayo ya usuluhishi,” alisema Balozi Mahiga.
Akiwasilisha ujumbe wa Rais Nkurunziza kuhusu hali ya Burundi jana, Spika Ndikuriyo, alisema serikali yao ipo tayari kufanya mazungumzo na wadau wote wa siasa kuhusu hali ya nchi hiyo na jitihada za kuumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea.
Akitoa maelezo ya kikao hicho kwa niaba ya Rais Dk. Magufuli, Balozi Maiga alisema Serikali ya Burundi imekubali usuluhishi unaofanywa na Rais Museveni, kwa niaba ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam Julai, mwaka huu, kwamba nchi hiyo iko tayari kushiriki katika mazungumzo hayo ya amani.
“Nimeagizwa nipeleke taarifa kwa mawaziri wa nchi za nje wa nchi jirani juu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yataanza kule Uganda Desemba 28 na Waziri wa Ulinzi wa Uganda amekabidhiwa jukumu la kuratibu mazungumzo hayo.”
Alisema suala lingine lililojitokeza katika mazungumzo hayo ni juu ya uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika kutaka kupeleka majeshi yake nchini Burundi baada ya siku tano, jambo ambalo Bunge la Burundi limepinga.
Balozi Mahiga alisema Burundi imepinga maamuzi hayo kwa kuwa inaamini kuwa hakuna dalili za kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ya Rwanda na kwamba kwa sasa kuna utulivu nchini humo tofauti na wasiwasi wa Umoja wa Afrika, jumuiya za kimataifa hasa Umoja wa Ulaya na kwa kiwango fulani Umoja wa Mataifa unaotoa msukumo wa kutaka kuyapeleka majeshi ya kulinda amani nchini Burundi.
“Wao kama Burundi wakiwa ni washirika wakubwa wa kulinda amani katika Bara la Afrika, wana wanajeshi 6,000 nchini Somalia, wanajeshi 1,000 Jamhuri ya Afrika ya Kati na dhamira yao katika kushiriki kuleta amani, wao watakuwa ni watu wa mwisho kuleta hali itakayosababisha hatari ya kutokea kwa mauaji yanayofanana na mauaji ya kimbari,” alisisitiza Balozi Mahiga.
Alisema kutokana na maelezo hayo, Rais Magufuli amependekeza kuwa Serikali ya Burundi ifungue milango ya mazungumzo na kukaribisha Umoja wa Afrika kupeleka ujumbe wa aina yoyote ili kwa pamoja watathmini hali ya usalama ilivyo nchini Burundi badala ya kukataa pendekezo hilo moja kwa moja.
Aidha, Balozi Mahiga alisema Rais Magufuli amemuagiza kwenda nchini Burundi kutazama, kujiridhisha na kutathmini hali halisi ilivyo hususan katika suala la amani hasa ulinzi na usalama wa raia katika Jiji la Bujumbura na maeneo mengine ya nchi hiyo ili kufahamu sababu zinazowafanya Warundi kukimbia nchi yao na kukimbilia nchi jirani ikiwamo Tanzania kama wakimbizi.
Aliongeza kuwa safari yake ya kwenda Burundi kwa kiasi kikubwa itasaidia kuendeleza mazungumzo yanayotarajia kufanyika nchini Uganda.
MSAADA WA MAREKANI
Katika hatua nyingine, Balozi Mahiga alisema Tanzania haikuwa tayari kuinyenyekea Marekani kutaka msaada wao kwa kile inachodai kwamba imeshindwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.
Mahiga alisema tayari Marekani imetoa sharti hilo na kwamba msaada huo utatolewa pale mgogoro huo wa kisiasa Zanzibar utakapomalizwa.
Alisema Tanzania ina utaratibu wake wa kidemokrasia, hivyo hawawezi kutekwa na presha za watu wengine kuvuruga utaratibu wao wa uendeshaji wa demokrasia hiyo kwa ajili ya kuhofia kupoteza misaada kutoka kwa wahisani.
“Tayari baadhi ya nchi zimeanza kutulalamikia kwamba ni kwa nini hatutangazi matokeo Zanzibar na wanatuambia kwamba sisi tunatatizo la kuminya demokrasia. Tumewaambia kwamba utamaduni wa kuendesha Demokrasia Zanzibar na uliopo Jamhuri ya Muungano ni tofauti,” alisema Dk. Mahiga na kuongeza:
“Hakuna nchi ambayo huwa inafanya uchaguzi bila migogoro, lakini sisi Tanzania uchaguzi umefanyika kwa amani isipokuwa huo tu wa Zanzibar ambao nao mazungumzo yanaendelea vizuri na tunaamini muafaka utapatikana. Hivyo tumewaambia wavute subira tumewahakikishia kwamba mambo yatakuwa mazuri watuelewe.
“Lakini kama hawatakubali hatuwezi kila siku kupiga simu kuwauliza jamani tumefikia hapa kwa hiyo ule msaada wetu upo au haupo, hapana.”
Kuhusu suala la kuwapo kwa taarifa za kuzuiliwa kwa hati za kusafiria za kidiplomasia, Dk. Mahiga alisema kazi inayofanyika hivi sasa ni kupitia hati hizo kwa watumishi hao.
Alisema wanafanya hivyo kwa sababu kumekuwapo na baadhi ya watumisi ambao wamestaafu kazi ambao walikuwa na hati hizo, lakini bado wanaendelea kuzitumia.
Chanzo Muungwana