Joyce Emmanuel: Asante Doris Mollel Foundation kwa Jengo la Watoto Njiti Kwimba. Nilipoteza Mtoto kutokana na Umbali

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
726
Reaction score
953
Mwanamke aitwaye Joyce Emmanuel James Mkazi wa Mtaa wa National uliopo Ngudu Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ameelezea jinsi alivyopitia changamoto tangu akiwa mjamzito hadi kujifungua Watoto wawili mapacha kabla ya wakati na kupelekea pacha mmoja kufariki ambapo amesema umbali wa kutoka Kwimba hadi Hospitali ya Bugando kufuata huduma ndio ulipelekea changamoto hiyo huku akiipongeza Taasisi ya Doris Mollel Doris Mollel Foundation (DMF) chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Doris Mollel kwa kuwasogezea huduma karibu baada ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa lenye viwango vya Kimataifa la kuhudumia Watoto njiti.
Your browser is not able to display this video.

Joyce amesema hayo wakati alipotembelewa nyumbani kwake na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk. Alex Ntale Gasasira, Timu ya DMF, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng’wilabuzu Ludigija na Viongozi wengine mbalimbali ambapo Joyce amesema kufuatia gharama za matibabu kuwa kubwa imemfanya afunge duka lake na sasa maisha yake yamekuwa magumu, anadaiwa kodi na anauguza Mumewe na Mkwe wake.

“Mimi ni Mama wa Watoto sita, nilibahatika kupata Watoto mapacha ambao nilijifungua nikiwa na ujauzito wa miezi 6 ambao walikuwa kilo 1.3 kila mmoja natarajia kupata Mtoto mwingine mwaka huu wawe saba, baada ya kujifungua waliniambia Watoto wamekaa mmoja kichwa chini mwingine miguu juu”

“Nikajifungua Mtoto wa kwanza Kulwa na Mtoto wa pili Doto nilihangaika sana, Kulwa alikuwa tu vizuri lakini Doto alikuwa na hali mbaya sana, wakaniambia twende Bugando maana hapa Zahanati hapakuwa na vifaa vya kuhudumia Watoto njiti, Kulwa akawa amepoteza, baadaye Doto wakampima wakasema humu sidhani kama kuna Mtoto mbona hapumui, tukawa tunarudi nyumbani tukijua amefariki njiani akapumua, tukaenda Bugando, alipofika kilo 1.5 tukaruhusiwa sasa hivi Mtoto ana miaka miwili na miezi, Bugando gharama nyingi tunaomba kama mmetuletea huduma hapa gharama zipungue”

“Nashukuru kwa kutuletea Hospitali Wilaya ya Kwimba tulikuwa tunahangaika kwenda Bugando kwanza kule ni shida hakuna wa kukuona, ningetamani nisaidiwe kiwanja au nyumba, maana nauguza Mume wangu na Mama Mkwe nilikuwa na kibanda biashara nimefunga”

Kwa upande wake Dkt. Alex na DC wa Kwimba wameiipongeza DMF kwa kufanikisha ujenzi huo, ambapo DC amesema “Jengo hili linaenda kupunguza uwepo wa Watoto njiti ambao wanazaliwa kabla ya siku, Mimi kama Msimamizi wa shughuli za Serikali ndani ya Wilaya nimeridhika na utekelezwaji wake , naamini kukamilika kwa mradi huu kutaokoa maisha ya Watoto wa Kwimba na wengine wa Halmashauri tano zinazotuzunhuka, tunawapongeza sana Wafadhili na Rais Samia kwa kufungua milangonya Wadau wengine wa maeneo kushirikiaa na Serikali kuokoa maishaya Watoto na Wajawazito”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…