Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,537
DODOMA: Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amedai kuwa ikiwa mradi wa maji wa Chigongwe katika Manispaa ya Dodoma utaanza kutoa maji ndani ya siku 21 atajiuzulu nafasi ya ubunge.
Selasini aliweka nadhiri hiyo juzi wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ilipofanya ziara katika Manispaa ya Dodoma na kutembelea baadhi ya miradi ukiwamo wa Chigongwe waliobaini kuwa na madudu.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo baada ya Kaimu Mhandisi wa Maji wa manispaa hiyo, Majuto Eriufoo kuomba kamati hiyo kumpa wiki mbili ili maji yaanze kutoka.
Kauli ya Eriufoo ikipingwa vikali na wabunge pamoja na mkurugenzi wa manispaa wakisema haiwezi kutekelezeka lakini aling’ang’ania kuwa itawezekana.
“Mheshimiwa mwenyekiti, tuwe wa kweli kwenye mambo ya msingi, mradi huu ukianza kufanya kazi ndani ya wiki tatu tangu leo lazima na nisisitize kuwa itakuwa lazima kwa mimi kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge,” alisema Selasini.
Chanzo: Mwananchi
====
Je, Joseph Selathini ataweza kusimamia kauli yake kama mradi utatekelezwa ndani ya siku 21?