Joseph K. Musukuma(Mb): Makonda awekwe ndani aseme anatoa wapi pesa ya kusafiri USA, UK na Dubai

lebara

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
646
839



Vyanzo vya Taarifa katika Kikao cha Bunge kinachoendelea jioni hii, Mbunge wa Geita Ndugu Musukuma amemtuhumu RC Makonda kuwa naye anahusika na dawa za kulevya.

Amedai kawa RC Makonda kwa mshahara wa U RC aeleze ni akina nani walimsafirisha kwenda Marekani na PARIS.

Musukuma ameenda mbele zaidi kasema Makonda aanze na kumkamata hawara yake aliyempangia Makongo.

Tuhuma za Makonda kusafirishwa likizo Nje ya Nchi na kuwa waliomsafirisha wanahusika na madawa ya kulevya hivyo anawalinda inaibua maswali mapya. Je nani anagharimia safari za Makonda Nje ya Nchi.

Hii vita ni kubwa ndugu zangu.

=====
UPDATES

Joseph K. Musukuma(CCM): Mawaziri wa Magufuli wamepigwa ganzi, wanamuogopa RC Makonda.

Joseph K. Musukuma(Mb): RC Paul Makonda mwaka 2015 alikuwa anaishi kwa Membe halafu leo ni Bilionea anamiliki VX na Maghorofa Mwanza.

Joseph K. Musukuma: Hata kama Makonda anachangiwa na wahisani, sheria inamtaka atangaze alivyopata pesa hizo. Achunguzwe na Vyombo vya Dola.
 
Asema vita ya madawa ya kulevya ni upumbavu .....

Anatoa wapi pesa na yeye anauza au na yeye anauza madawa ya kulevya?

Asema makonnda anafanya usanii wauza madawa wakubwa anawajua na anashiriki nao kufanya kazi aache usanii.......
 
My take : Na huyu msukuma akamatwe kwa uchochezi...........
 

Attachments

  • tapatalk_1486374688965.jpeg
    tapatalk_1486374688965.jpeg
    69.4 KB · Views: 178
Akae atulize boli hawa watu nahiai wanatumiwa ili kumtoa Makonda kwenye leli kama anahusika ajiandae tu zamu yake itafika atulie tu Makonda kaza hapohapo watu wameshaanza kujitaja kwa staili nyingine
Hatakuandika kiswahili huwezi kuandika ndugu yangu kuchambua hoja nzito kama hizi utaweza kweli,makonda amebugi tena sio kidogo asante ccm kwakung'arisha njia kwa upinzani
 
Back
Top Bottom