Jose Mla vichwa ni hatari.

Jose Mla vichwa ni hatari.

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
23,877
Reaction score
31,632
Dah huyu jamaa anakula almost kila kiumbe kinachopita mbele yake, iwe chatu, paka, panya, kenge nk

Japo asilimia kubwa video nyingi anapost anakula kenge na panya.

Anakuja kwa kasi sana kwa sasa naona ameshaanza kupata wafuasi kadhaa, ule uoga na kinyaa cha watu kula panya umeanza kuondoka taratibu taratibu na kuona ni msosi wa kawaida.

Kula panya sio big issue sana maana hata wamakonde wanakula tangu enzi na enzi, ila ulaji wa kenge, paka, chatu aisee unashtusha sana.

Kenge wengi wanamuogopa kutokana na kusifika kuwa na sumu kali ila jamaa naona hajàli hilo yeye anatafuna tu kwa kwenda mbele.

Aangaliwe kwa makini huyu asije akatuletea magonjwa ya hovyo , hiyo kula kula yake itaponza jamii kama wale watu wa kongo wanavyoongoza kuwa na magonjwa mengi hatarishi kutokana na ulaji wao wa kila kiumbe kinachopita mbele yao.

1000019983.jpg
 
...Usikute anakula hadi vidume msawazo...
Mmesema Hana kinyaa😝
 
Panya (Ndezi)
analiwa na wamakonde, wasafwa, Wamalila, Wazaramo , Wandengereko, Wamwela.

Chatu
analiwa na Wangoni, Wandendeule, Wamanda, Wayao,Wakisi.

Kenge
Awe Mbulu au Maji analiwa na Wazaramo, Wandengereko, Wanyagatwa, Wakwele, Wazanzibari, Wamatumbi, Makabila ya Morogoro, Wamakonde.

Hivyo jamaa yupo sahihi vyakula vingi vinaliwa kasoro ni tamaduni tu
 
Waarabu wanakula sana kenge tangu enzi na enzi
Nimeshuhudia kwa macho yangu wakiwa wanakula
Nyama ni nyeusi sana na haina sumu
Ila ni mgumu sana kuiva inachukua mda

Halafu hata ukiwa unapakua bado nyama inatetemeka
Kuhusu chatu au Nyoka wakubwa pia wanaliwa sana sehemu nyingi duniani

Pia nimeona huko Thailand na majiji mengine wakila na hata kunywa damu yake

Duniani kuna mambo huyu cha Mtoto maana amepunguza gharama za maisha tu
 
Aisee, kumbe
 
Aiseee
 
Mimi siwezi shangaa.
Unajua mfano kuna nchi kitowewo kama ng’ombe,mbuzi,kuku na samaki wanaojulikana kuna nchi ni hadimu au kutopatikana kabisa.
Sasa vilivyopo vinaweza kuwa kitowewo mfano kuna nchi hakuna mboga nyengine zaidi ya samaki.
 
Kuna mzungu mmoja hapa 🇬🇧 yeye kazi yake ya kujipatia riziki ya mlo ni barabarani tu kwa miaka zaidi ya 30

Aliwekwa mpaka kwenye Tv

Anazunguka kutafuta mizoga iliyogongwa na magari
Kuanzia fox 🦊, karunguyeye, ndege wakubwa na wadogo badgers na chochote atakachopata siku hiyo

Je nani anaweza kuokota mzoga wowote na kula?
 
Wewe ndio hatari kwa mfano Mimi nimekulia mazingira ya watu wanaokula panya,mende,sisimizi,nge au nyoka inakuaje?
Wanyama wote na wadudu Wana virutubisho ila epuka wenye sumu TU yaani poison kama Wana venom mfano nyoka kata kichwa kula protein na ma vitamins
Unafeli wapi nigga
 
Cha aajabu unakuta sio asili yake kufanya hivyo

Ila anafanya hivyo kwa ajili ya kupata umaarufu

Humanity is a mystery
Asili ndio jnini? Dini tu ndio zimetugeuza mazombi. Waislam tunakatazwa hadi kula kambale eti hana magamba.
Kuna samaki wanafana na nyoka kabisa ila wanaliwa ila nyoka eti haliwi kisa eti nyoka ni shetani.
Nenda Feli utakuta vidudu vya ajabu lama kaa wanaliwa ila konono tusimle. Senene aliwe ila panzi tusimle.
Sababu kubwa ni ukoloni wa fikra za azungu na warabu hakuna kingine.
Punda kama punda tusimle, kwa sababu gani ?
Huyu jamaa nampongeza kufanya decolonization of whitewashed mind.
Kwa sasa kuna uamsho mkubwa sana wa kuanza kuhoji kila upuuzi wa mzungu na mwarabu na utapuuzwa si mda mrefu na watu kurudi kwenye asili. Asili ni kama hadzabe life sio hio ya wazungu.
I'm telling you tutarudi kula hadi nyasi walizokuwa wanakula babu zetu. Ng'ombe anaishi kwa majani ila sisi wazungu wametupanga. Tunaweza kuishi hata kwa kula majani na mizizi.
 
Wasiomla kambale ni wasabato na sio waislamu.

Mbali na kambale ,hawamli pia ngamia.
 
Back
Top Bottom