Jordan yaapa kupambana na Islamic State

Jordan yaapa kupambana na Islamic State

Bome-e

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
17,247
Reaction score
26,394

150203215650_jordan_king_abdullah_144x81_reuters_nocredit.jpg

Mfalme Abdullah wa Jordan

Mfalme wa Jordan ameahidi mapambano yasiyo na huruma dhidi ya wapiganaji wa Islamic State kufuatia kuuawa kwa rubani wa nchi hiyo.

Baada ya mkutano wa makamanda wa juu wa jeshi na maafisa usalama, Mfalme Abdullah amesema vita hivyo vitaelekezwa dhidi ya kundi hilo na damu ya rubani huyo wa ndege za kivita Muath al-Kasasbeh haitapotea bure.

Hapo jana, Jordan iliwanyonga wafungwa wawili wapiganaji wenye msimamo mkali waliokuwa katika orodha ya adhabu ya kifo, kama kulipiza kisasi cha kuuawa kwa rubani wake huyo.

Miongoni wa walionyongwa ni Sajida Al-Rishawi, ambaye wapiganaji wa Islamic State walitaka aachiwe kama sehemu ya kubadilisha na mateka huyo wa Jordan waliokuwa wakimshikilia.

Katika hatua nyingine kundi la wabunge wa Uingereza limeitaka nchi yao kuchukua hatua zaidi kupambana na kundi hilo la Islamic State.

Ripoti kali iliyotolewa na kamati ya Ulinzi ya bunge hilo imesema maafisa na maafisa waandamizi wa jeshi wameshindwa kuanzisha mikakati iliyowazi kufikia malengo ya kuwashinda wapiganaji hao wenye msimamo mkali.

Awali serikali ya Uingereza ilisema hatua zinazochukuliwa za kutoa msaada wa kijeshi ni moja ya sehemu ya mikakati ya ulimwengu kupambana na kundi hilo.


Chanzo:
BBC
 
v3-Sajida-al-Rishawi-2.jpg ISIS wailikuwa wanataka hiki kibibi (Sajida Al-Rishawi) kiachiwe ili kije kuendelea kuleta maafa
 
Waache waende tu,, ila wakikamatwa na kuchomwa moto au kukatwa vichwa kelele zinaanza oooh ISIL... dunia imekaa kinafiki sana, USA ni baba wa yote haya kwa kigezo cha demokrasia,, Binadamu yoyote akiacha unafiki na kufuatilia haya basi ataujua ukweli wa haya,, kwani wairaq walivyoishi chini ya Saadam haya yalikuwepo?? Je libya demokrasia imepatikana???
 
[video=youtube_share;zYQEU9y1z4I]http://youtu.be/zYQEU9y1z4I[/video] Jamaa wameamua kuwamaliza ISIS sasa, wakati wao ndio waliwapa training pamoja na Israel, USA si ajabu hio. Any way Good step.
 
Back
Top Bottom