Mkuu nimetembelea tovuti yako, tatizo kwako ni kuwa Login form imepotea, na si lolote. Hii inawezekana imeshambuliwa na chrono form au wewe mwenyewe bila kujua ulidisable llogin form.
Kutatua tatizo:
1. Tumia FTP kwa kubadilisha $offline = '0'; na kuwa $offline = '1';
2. Nenda kwenye database (tumia PHP Admin inayopatikana kwenye host wako), nenda kwenye table inayoitwa _modules chini utaona kuna module inayoitwa Login. Kumbuka kuna login za aina mbili, moja ni kwa ajili ya user (front end ) na nyingine kwa admin. Ili kuwa salama pia sijui umeenable login ngapi ndio maana nilikushauri uiweke offline, enable modules zote za login kwa kuset published kwenda moja.
3. Login na uondoa usichotaka na kuirudisha site online
Kama vp unaweza nitumia PM details za server yako nikusaidie bila gharama yoyote.