Joomla East Africa Community

Kilongwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
423
Reaction score
116
Tovuti hii ya Joomla Afrika ya Mashariki imeanzishwa ili kuwapatia jukwaa la majadiliano, elimu na maarifa juu ya Joomla kwa watumiaji wake kutoka ukanda huu. Neno Joomla! limetokana na neno la Kiswahili "Jumla" hivyo kuna umuhimu sisi kama watumiaji wa Kiswahili kuikumbatia Joomla, kwa kufanya hivi, sio tu tutaweza kuonesha umuhimu wake, bali pia itatuwezesha kuifahamu joomla ipasavyo tutaweza kupiga hatua kwenye matumizi yake ipasavyo.
Ndani ya Tovuti ya Joomla Africa Mashariki, utaweza kujifunza kwa njia ya Video, Makala mbalimbali toka kwa waandishi waliobobea kwenye matumizi ya Joomla pia utaweza kujadiliana na watumiaji wenza kwenye jukwaa la majadiliano.

Jukwaa hili pia ndio limewezesha kutafsiri joomla na kuwa Joomla ya Kiswahili.

Tembelea Joomla Afrika Mashariki - Elimu na Maarifa ya Joomla
 

ni official joomla site ama ni nyie afroit mmeijenga kusogeza awareness ya matumizi ya joomla afrika ya mashariki?
ntajiunga ili nitoe michango yangu kwa kadri ntakavyoweza
 
Reactions: hbi
Hii ndio itakuwa Official Joomla kwa Afika mashariki, kwani tumeonelea ni vyema tukatumia Afrika mashariki kuliko kuchukua kila nchi kivyakevyake. Kwa sasa tupo kwenye harakati za mwisho za authorization kabla kuwa official Joomla EA, pia mmoja wa waanzilishi wa wavuti hii ndiye Official Joomla Swahili Translation Coordinator Mr Khassan (Toka Kenya).

Karibu sana C6, kwani sisi kama wasomi inabidi tuact kivitendo (sio siasa) na tushirikiane kwa pamoja, kwani Tz wengi tuna kasumba ya kuwa nataka MIMI nionekane, kitu ambacho kinarudisha nyuma mambo mengi.

Kama ilivyo kwenye sheria za Joomla, hii site (project) ni NON PROFIT, ni kwa ajili ya kushare ujuzi, maarifa nk.
 
Dah kufanya kazi na majirani zetu ni kazi aisee, ni FULL kujimegea, napenda kusema tumefikia uamuzi wa kuiterminate project ya Joomla East Africa, sababu kuu ni kubanwa kwa masilahi kama Mtanzania (Si kama Kilongwe). Baadhi ya babu ni hizi;

1. Lugha ya kiswahili iendelee kubakia sw-KE badala ya sw-EA

2. Kutowaalika watu wengine kwenye uchangiaji wa makala

3. Server na domain zote ziwe kwa muhusika mkuu ambaye ni Mkenya

4. Kuwa na limit za utumaji wa makala (kwakuwa muhusika wa pili aliona hatoweza kutuma makala hivyo akasema kwa mwezi kuwe na makala mbili tu kwa kila mtu, hivyo akaona kama atazimwa) na kwenye makala nisimention Tz.

5. Kwakuwa Kiswahili kilichotumika sicho, nikashauri watu wapewe access ya kutafsiri, kwakuwa muhusika aliona kama watu wengine wakiingizwa atatakiwa awaacknoledge, akaleta kisingizo kuwa Joomla wamekataa (asif tunaishi kwenye ulimwengu wa 1960)

na mengine meengi.

Hivyo nimeonelea ni vyema tutakuza AfroIT na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi. Hivyo tuendelee kwenye AfroIT.
 

Awww! Huo Ubinafsi umepitiliza.
Nitakupa idea....!
Just make it "Unofficial Joomla EA" na hakuna atakayekufunga na hautahitaji kuomba chochote kwa Yoyote.
Nimeku PM mpango mkakati flani. Check PM.
 

mkuu ungefanya kama operamini ya kiswahili kwani zipo mbili cha kenya na tanzania ili kufanya joomla ya kiswahili iwe ya ke na tz mbona kuna english ya US na UK try it dude..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…