hiyo bold inaonyesha kuwa yote uliyoyaandika ni uwongoHivi karibuni Dr. Kitilya Mkumbo alisema kuwa Johnson Mashaka anagawa fedha kama njugu!
wakati akitoa mjdadal huo, wadau wa JF wakawa hawana uhakika na chanzo cha data hizo; hata baadhi ya wakazi wa Jimbo la Ukonga - JF wakawa hawana lao.
Katika uchunguzi wangu niliofanya nimegundua yafuayo:
- Ni kweli Mh. Makongoro Mahanga amekuwa akifanya vikao vya siri katika kata za Tabata, Segerea, Kitunda na Kipawa, ili kulinda kitumbua chake cha Ubunge.
- Johnson Mashaka ambaye amesafiri siku ya J'5 tarehe 9 Sept kurudi marekani, ameweza kukutana na wadau wa ccm wa jimbo la Ukonga ili kujiadaa vyema.
- Johnson Mashaka + Makongoro Mahanga wote ni wakazi wa Kata ya Segerea.
- Wote ni kabila la wajaluo.
- Ni wazi Kuwa mojawapo ya vijana vichwa hapa Tanzania ni Johnson Mashaka! Ni mtaalamu wa masula ya kompyuta wa kutegemewa na kampuni mkoja - Texas.
- Makongoro ameongea na baadhi ya wadau wengine wa ukoo wa "kijaluo" ili kuongea na kijana aende akagombee jimbo la Rorya! Tayari wadau wamekataa kwani Prof. Sarungi ana mpango wa kurudi jimboni tena.
- Maongoro amekiri kuwa kijana pekee ndani ya ccm anayeweza kumsumbua kwenye kura za maoni ni Mashaka.
- Ni wazi kuwa Mashaka kama kijana makini, kugombea kwake kupitia CCM inaweza kuhoji uhalali wake na umakini wake katika uchaganuzi na uchambuzi wa fursa za kisiasa!
- wasiwasi wangu ni dogo huyo kuanza kuhonga fedha inaondoa uhalali wake wa kusemwa kuwa "zaidi ya Zitto"
- Namshauri agombee kupitia Chadema - ingawa nasikia kuna utitiri wa wagombea - Mwita waitara, Binagi, Dady na wengine wengi..
- Naungana na uhakika wa hoja za Kitila Mkumbo!!
Aibu ya karne itatukumba wana Jamii Forums pale itakapojulikana kwamba bwana mdogo wala hakuwa na nia ya kugombea Ubunge....
Aibu ya karne itatukumba wana Jamii Forums pale itakapojulikana kwamba bwana mdogo wala hakuwa na nia ya kugombea Ubunge....
Mkuu, marekebisho kidogo tu.Huyu Nape wako hafui dafu kwa Myika huko Ubungo afadhali angekwenda Temeke anaweza kuambulia!! Ubungo wamejaa wasomi wasioweza kurubuniwa na propaganda za CCM!!Kama Nape haamini ajaribu aone atakavyogaragazwa.
Kwa kuongezea tu Mkuu. Kata nyingine ni Chanika.- Mkuu kila unapofungua kinywa unazidi kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulipoanzia na kuishia, kila siku unalia lia hapa kwamba Kyela unaibiwa na kuongozwa na mafisadi, hivi kweli unaweza kulinganisha maendeleo ya jimbo la Ukonga na Kyela?
- Mkuu jimbo la Ukonga lina kata nyingi zikiwemo za Kinyerezi, Kipunguni, Kitunda, Ukonga Magereza, Majumba Sita, Sitaki Shari, Segerea, Airwing na zinginezo, sasa hebu nitajie kata moja tu kati ya hizi unayoweza kulinganisha na hata jimbo zima la Kyela kimaendeleo?
Masahihisho: Amekaa Bungeni miaka 10 akiwa Mbunge wa Ukonga. Kati ya hiyo, ni miaka minne tu ndio amekuwa katika serikali.- Ndio kwanza tumefungua bara bara mpya ya lami, kutoka getini Airwing yaani njia panda ya Airport mpaka gerezani Segerea kufikia Tabata unaunganisha mpaka Kimara. Mahanga sio siri ni kiongozi mchovu, lakini Ukonga sio Mahanga ambaye amekaa bungeni kwa miaka minne tu so far, hili jimbo ni bomba kabla hata yeye kuhamia Ukonga.
- Eti mkuu jimbo lenye vitega uchumi na kutoa ajira kwa wananchi jimboni kama Julius Nyerere International Airport, FFU HQ, JWTZ-Airwing HQ, JWTZ-Mizinga Squad, Gereza Kuu la Ukonga, Gereza Kuu la Segerea, Viwanda vya nguo Kiltex na Sungura tex, Kiwanda maalum cha kutotota vifaranga vya kuku, Segerea Catholic Seminary, unasema unaweza kulinganisha hili jimbo na Kyela? Hivi unajua hili jimbo lina secondary ngapi mkuu? Hebu nitajie jimbo moja tu Tanzania nzima linaloweza kulifikia jimbo hili la Ukonga kwa maendeleo?Nyongeza kidogo: kuna chuo cha Materials Management.
Na familia ya Mkuu wa Magereza mstaafu Oneil Malisa. Na complex estate, a.k.a. future makazi ya Recta.- Na pia jimbo hili tunajivunia sana kwa kuwa na kata ninayotoka ya Kinyerezi/Sitakishari ambayo ni a home for national celebrities kama the sitting national leaders Waziri Wasirra, Mkuu wa Itifaki Balozi Itatiro, RC wa sasa Mbeya Mwakipesile, Mbunge wa Kawe Rita Mlaki, Managing Director Azania Bank Charles, Managing Director Wananchi Bank Mzee Mkwawa, pia tuna wastaafu wa taifa kama familia ya waziri wa zamani wa afya Mzee Sterling, Mzee Apiyo, familia ya marehemu Waziri Itatiro, familia ya marehemu makamu wa mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Ngwilulupi, familia ya Balozi wetu wa zamani Nigeria Marehemu Mwasakafyuka, Wakuu watatu wa zamani wa Magereza Mzee Mwanguku, Mzee Mwaijande na Mzee Mwaipopo, familia ya mkuu wa polisi zamani marehemu Mzee Liani, Pia tuna wafanya biashara maarufu kama kina Mujuluzi, majority owner wa Imma, Dr. Mwaijande owner wa pharmacy maarufu pale Muhimbili hospital, kampuni kubwa ya mabasi na malori ya Mahende, Club maarufu sana Dar ya Hill-teck, pia ni a home for a former Simba player/national team Idd Pazi "Father" na pia ni a home for mimi mwenyewe Mukulu Field Marshall Es, yaani wazee wa sauti ya umeme! na Mkulu Mashaka John.
I conquer, Sir. Kinachoendelea Ukonga si cha kukiachia kipotee.Wakuu Malafyale, Sinkala na Mkandara huuu ni wakati wa kuhamishia hii elimu tunayoipata hapa JF, katika jimbo letu badala ya kurushiana maneno machafu yasiyo na mshiko kwa masilahi ya taifa kama hao wa Kyela, na ni lazima tujihusishe sana na hii process ya kutafuta mbunge anayefaa kwa jimbo letu yaani wa kuendeleza aliyoyakuta, mimi toka jana nilipoiona hii habari ya Mashaka, nimekua nikiwasiliana na wazee wa jimbo kujua kinachoendelea na soon tutaweka msimamo hapa. Mkuu Engineer karibu sana jimboni kwetu ujifunze elimu ya maendeleo ya jimbo mkuu.
Respect.
Field Marshall Es!