John Pombe Magufuli International Airport

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
17,365
33,004
Wakuu nina wazo napenda ku-share na nyie....

Kwa sababu Mzee baba anapambana sana kuboresha maisha ya Wana Chato, basi kwa heshima na taadhima na itifaki yote ikizingatiwa napendekeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato ubadilishwe jina na uitwe John Pombe Magufuli International Airport ili kuenzi mchango mkubwa wa huyu mwanachato katika kuleta maendeleo jimboni Chato kwa ujumla.

Ni matumaini yangu kuwa wenye mamlaka na wazee wa "ndiyo mzee" watachukua hili wazo na kulifanyia kazi.
 
Pia wasisahau uwanja mpya uitwe John Pombe Magufuli International Stadium
 
Pia wasisahau uwanja mpya uitwe John Pombe Magufuli International Stadium
Pita barabara ya kutoka Chato kwenda Muleba uone jinsi kila shule ya msingi na sekondari 'zilivyogombania' kuitwa jina lake, tena kipindi hicho akiwa bado mbunge/waziri tu. Ikabidi sasa shule zitofautishwe kwa namba..Magufuli 1, 2, 3, etc.
Unabaki kujiuliza hivi hakukuwa na majina mengine mpaka kila shule iitwe Magufuli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom