PreGE2025 John Mrema: Madai ya kuwa nimekimbia na YouTube na X za CHADEMA si kweli, sikuwa hata na Password ya hiyo Mitandao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Baada ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche kueleza kuwa Akaunti za chama za X (Twitter) na YouTube zimechukuliwa na John Mrema na kudai alikuwa akipata faida binafsi kupitia mitandao hiyo ya chama, Mrema ametoa ufafanuzi upande wake.

John Mrema ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA amezungumza na JamiiForums kuhusu tuhuma hizo na kueleza kuwa hazina ukweli.

Kusoma alichokisema John Heche, bofya hapa ~ John Heche: John Mrema amekimbia na Akaunti za YouTube na X za Chama, tuligundua kila wiki analipwa Tsh. Milioni 3

JOHN MREMA: WANANICHAFUA, SIKUWA HATA NA PASSWORD YA MITANDAO YAO
Hizo taarifa sio za kweli na hata wao (CHADEMA) wanajua sio kweli, ni propaganda tu, mimi nilikuwa mkuu wa kitengo lakini sikuwa na ‘access’ ya kupost chochote, kuna vijana ambao ndio walikuwa wanafanya hiyo kazi na ndio ambao wapo nao mpaka sasa.

Sina hata password ya hizo akaunti wanazozitaja, nilipokuwa nikitaka kupost taarifa, niliandaa na kuwapa vijana hao waiposti, hata Katibu Mkuu naye alifanya hivyohivyo, sisi hatukuwa watu wa kuposti hata mara moja.

Ukitaka kuamini hilo, mimi niliondoka Januari 2025 lakini hadi Aprili 2025 akaunti zilikuwa zinafanya kazi na walikuwa wakizitumia wao (Uongozi uliopo madarakani kwa sasa), kilichotokea kwa taarifa nilizonazo ni kuwa…

Siku ambayo Mwenyekiti wa Chama chao anakamatwa kulifanyika majaribio kadhaa ya kuingia kwenye akaunti ya Twitter (X) kwa kukosea, hivyo akaunti ifungiwa kwa muda na taarifa kutumwa katika email iliyotumika kufungulia hiyo akaunti.

Hilo wanalijua na walielezana kwenye vikao, Mnyika anajua, Heche anajua na Apolo ambaye alikuwa na access na hiyo akaunti anajua.

Kuhusu YouTube ambayo ilikuwa inaendeshwa na Abulkarim ambaye ana madai yake, akawaeleza wamlipe, Heche akamwambia hayo madai yake ni makubwa wataangalia namna.
 
Tusubiri majibu ya Heche... ningekuwa na media ningewaita kwenye interview tujue mwongo nani.

Au akahojiwe AbulKarim atatuambia liongo ni lipi.
 
  • Thanks
Reactions: Tui

mropokaji heche ni muongo siku zote :pulpTRAVOLTA:
 
CHADEMA inapita katika kipindi ambacho ilitakiwa kuongozwa na busara na ukomavu kuliko mihemko ya balehe ya kisiasa!
 
Kweli kabisa, Heche muongo sana
Nimesema Heche anaanza kuwa muongo,ila ni vyema ajue hata mwenzake alianza uongo na akafanikiwa kupata kiti kinachomtesa kwa vurugu za kila namna na misukosuko ya kila aina
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Chadema huwa ni wataalamu wa kutengeneza stori za uongo zinazofanana na ukweli, wakiamua kutafuta public sympathy ni sekunde moja tu utazushiwa suala la uongo linalofanana na ukweli.

Chadema na Majizi ya Ccm wote siyo watu wa kuwaamini.
 
Kweli kabisa, Heche muongo sana
Mna majibu rahisi utazani mpo ndani ya chama ila ya CCm kama mpo sokoni mfahamu kuna mtu naibu waziri kasema yeye ni mafia anaweza kumaliza yoyote ni mwana CCM wenu
 
Heche asiingie kwenye huu mtego wa tuhuma akumbuke objective yake haikuwa G55, mwisho atajikuta tayari yupo kwenye dimbwi la vita na G55 na kugawanya nguvu zake. Sio kila vita vya kupigana, vingine unaacha kwanza.

Una vita na chama tawala, una vita na serikali ifanye reform, una vita na OCD, una vita ya kuimarisha chama sababu watu wanaondoka, mkubwa wako yupo gerezani anategemea wewe uliye nje upigane, bado unaletewa sahani nyingine ya vita unaiparamia unaitaka ilihali vita na chama tawala na serikali pekee ni mziki mnene, mzito mpana haswa unaoweza kukuchezesha mpaka utanuke uchanike iwapo hutokuwa na akili nyingi.

Mfano Mrema akifungua kesi tayari anaanza kumkeep busy na jambo lisilo objective yake ya msingi.
 
Muda mwingi

Hakika wewe ni mshauri wa maana,mbona alishahama kwenye vita halisi sasa hivi anapambana na vita asiyoijua!!?Watu wanatumia sana akili kwenye vita sio nguvu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom