PreGE2025 John Mrema: CHADEMA 'imeuzwa' ndiyo maana tumeondoka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mkurugenzi wa kurugenzi ya Habari na Taarifa kwa Umma wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema amedai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) 'kimeuzwa' kwa watu wasiokuwa na mizizi na uchungu wa chama hicho ambacho amekieleza kukosa mwelekeo.

Mrema ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya Jumatano Juni 04, 2025, Mjini Musoma mkoani Mara katika mwendelezo wa Operesheni ya CHAUMMA For Change (C4C).

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Chama chenu leo kimekabidhiwa kwa mtu aliyeishi Ikulu maisha yake yote mpaka alipostaafu, akajiunga nacho 2015, Edward Lowassa akampendekeza awe mbunge, wenzake wawili walisharudi CCM, yeye kumbe alibaki kimkakati, leo kakabidhiwa CHADEMA, ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, halafu mnasema chama hakijauzwa, nendeni mtafakari", ameeleza Mrema.

Your browser is not able to display this video.
 
Huko Serengeti wamezomewa na kidogo wapigwe mawe na wakurya 🤔🤔🤔

View: https://youtu.be/O_ZKzfhlr6A?si=qWAObtkT-eGcddwO
Halafu waandishi wa habari wamekula pesa sana. Cheki hizo kamera zote eti yote hii ni kujaribu kupromoti kinyesi (mavi) yasiyouzika
 
Huyu aliyemroga kamuweza kweli
 
John Mrema tulikuwa wote Chuo Kikuu ila sikuwahi kujua ana upeo mdogo kiasi hiki!
Sasa Ruth Molell kuwa Mwenyekiti wa Bodi Kuna shida gani?
Kwanza Mama Ruth Molell ni mama mwenye weledi na integrity kubwa sana na CHADEMA kuwa naye ni hazina.
Hakuna Jimbo lolote John Mrema anaweza kusimama na kushinda UBUNGE katika JMT.
 
Haahaa ndo maana akatapeli na account za chama za you tube kupitia chadema media?
 
Mrema kaharibika ubongo
 

Fundi Nchundo, Nyanye Go, Fortila, Drlfter, binti viziwi na wale wengine, yale mambo yetu na madalali.

Kazi kweli kweli.
 
LISSU impact amefanya Mrema amekua na akili za Mtoto wa Chekechea
Yaani ujio wa Lissu ni kama Horror movie pale Chadema. Unakumbuka picha ya Kigaila akiwa anampatia fomu Lissu? Basi ule ndio muonekano wa akina Salum Mwalimu, Mrema, Ntobi na wengine ambao maslahi yao yalikoma siku ya uchaguzi ile Januari, baada ya uchaguzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…