PreGE2025 John Mnyika: Taratibu za Uteuzi wangu zilifuatwa, Wanachadema msiwe na wasiwasi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Your browser is not able to display this video.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika ametoa ufafanuzi na kujibu hoja kuwa taratibu za Kikatiba zilikiukwa wakati wa uteuzi wake katika nafasi hiyo kwa kusema taratibu zote zilifuatwa na kwamba kinachofanyika ni mbinu haramu na kwamba watazidhibiti.

Mnyika amesema mambo hayo yanafanyika kutaka kukitoa chama kwenye ajenda yao ya NO REFORM NO ELECTION.

Amesema hayo leo tarehe 25 Machi 2025 wakati akifungua mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa BAWACHA na BAVICHA kutoka Kanda ya Kusini. Mafunzo hayo yanafanyika Masasi, mkoani Mtwara. Katibu Mkuu amembatana na Mkurugenzi wa Mafunzo, Oganaizesheni na Uchaguzi John Pambalu katika mafunzo hayo.

Ikumbukwe, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa muda wa Wiki moja kufikia Machi 31, 2025 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwasilisha maelezo kuhusu malalamiko ya mjumbe wa Baraza Kuu wa Chama hicho, Lembrus Mchome.

Lembrus Mchome ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mwanga, alimuandikia barua Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya uchunguzi juu ya uhalali wa Kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichofanyika Januari 22, 2025 na kumpitisha John Mnyika kuwa Katibu Mkuu wa Chama.

Mchome alisema kwa utaratibu wa Chama, wanaoshiriki Baraza kuu ni Wajumbe pekee na sio wawakilishi lakini siku ya Baraza kuu palikuwa na Watu ambao si wajumbe na walishiriki kupiga kura.
 
Mkuu heading ina nyama nyingi kuliko content... rekebisha hili tufaidi habari
 
Haya Msajili eleza wana CCM na umma wa watanzania kwamba CCM walitumia kanuni na vifungu gani vya katiba yao kumpitisha Samia kuwa mgombea Urais na Makamu wake Nchimbi??

Afu yule mwanachama aliyefungua kesi mbona umekaa kimya?? Yenyewe haikuhusu??
 
Ushahidi, amesema wp?
 
Msajili ana record ya kununua ugomvi, matokeo yake anakuja kuonekana……..
 
Unajua bodi ya ligi na msajili wa vyama ni mtu na mdogo wake!
HAMUWEZI NIELEWA LEO, IPO SIKU MTANIELEWA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…