John Mnyika amepotosha umma

John Mnyika amepotosha umma

Joseph Ludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
384
Reaction score
508
John Mnyika, ameongea na vyombo vya habari leo.. Kama kawaida ya chama chake kasambaza uongo, upotoshaji na visingizio. Alisema atatoa hoja tatu lakini ametoa zaidi. Tutazipitia hapa na kuonyesha upotoshaji wake.
Hoja namba 1 : WAGOMBEA WA CHADEMA WAJAZE FOMU HARAKA NA KUKUSANYA.
Kutokana na mabadiliko ya ratiba ya uchaguzi, Mnyika ametoa wito kwa wagombea wa chama chake wajaze haraka fomu na kuzirejesha kabla ya tarehe 1 Novemba 2024 ambayo ni siku ya nwisho. Tatizo kwenye hoja yake hii ni kuwa, hajagusia suala wala haja ya wagombea kujaza fomu kwa usahihi na kwa kufuata matakwa ya kisheria. Matokeo yake wagombea wataharakia kujaza na watakosea kisha watawekewa mapingamizi na kuenguliwa. Ikiwa hilo litatokea, wa kulaumiwa ni Mnyika mwenyewe.

Hoja namba 2 : UDHAMINI KUFANYWA NGAZI YA CHINI.

Mnyika anapinga jambo hili akitaka wilaya za Chadema ndiyo zidhamini wagombea wa vitongoji. Amefikia mpaka kuandika barua kwa Wasimamizi. Hii ni kwa sababu CHADEMA haina uongozi kwenye wikaya zote, haina kabisa uongozi kwenye kata, na kwa hiyo kwenye vitongoji.

HOJA namba 3 : Mwakala wa CHADEMA kufanya fujo vituoni

Mnyika anasema mawakala wa Chadema wasisubiri utaratibu wa kisheria bali wajichukukie sheria mkononi na kuchana madaftari ya kujiandikisha ama kuwapiga waandikishaji ikiwa wataona kuna ukiukwaji wa sheria. Hapa Mnyika anataka kuleta vurugu kwenye vituo na kuharibu mchakato wa uchaguzi

HOJA NAMBA 4: KUBISHIA TAKWIMU ZA WAZIRI
Mnyika amefikia kubishia takwimu za waziri. Inawezekanaje mtu kubishia takwimu zilizotolewa. Leo ni siku ya 6 ya zoezi hili. Kwa mujibu wa Mnyika ni kwamba uandikishaji umefikia asilimia 45. Mnyika anakataa eti ziko chini zaidi. Ana maslahi gani ikiwa watu hawaandikishwi?

Mnyika amekata tamaa. Anaona chama chake hakina uwezo wa fedha wala watu kuendelea na uchaguzi wala kushinda. Anataka auharibu uchaguzi ili tukose wote. Uchawi huo.
 
Mnyika bwana. anambishia wazir ambae anapokea taarifa kila siku za nchi nzima juu ya zoezi zima la uandikishaji! wakati CHADEMA wameshindwa kuweka mawakala nchi nzima kwenye vituo ambao ndoo wangewapa taarifa sahihi juu ya zoezi la uandikishaji. Sasa labda atwambie katumia utaalamu gani kupinga taarifa ya waziri
 
Hapa vipi?
IMG-20241017-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom