PreGE2025 John Mnyika aligombea ubunge 2010 kwa mara ya kwanza

PreGE2025 John Mnyika aligombea ubunge 2010 kwa mara ya kwanza

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu,

Ni kweli Mnyika alifanya hivyo mwaka 2010? nataka kujua ukweli wa hii taarifa?

Mnyika LLB.jpg

 
Tunachokijua
John Mnyika ni Katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA amewahi kuwa pia mbunge wa jimbo la Ubungo 2010-2015 na baadaye jibo la Kibamba 2015-2020.

Madai

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram Juni 20, 2025 alichapisha taarifa kumhusu Kaimu katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika na Kiongozi mstaafu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Taarifa hiyo imeeleza baadhi ya mambo ikiwemo kuwa kwa mara ya kwanza Mnyika aligombea ubunge mwaka 2010 miaka mitatu baada ya kumaliza chuo. Pia taarifa hiyo inaeleza kwamba Zitto alihamia ACT-Wazalendo mwaka 2015.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa baadhi ya sehemu katika taarifa hiyo ni zinapotosha.

John Mnyika alianza kujihusisha na siasa akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu na aligombea kwa mara ya kwanza ubunge akiwa na miaka 24-25 mwaka 2005 akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akishindana na Charles keenja kutokea CCM ambapo alishindwa.

“Nikaingia kugombea kwa mara ya kwanza mwaka 2005 nikagombea ubunge. Wakati nagombea mwaka 2005 nilikuwa bado mwanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam” - John Mnyika

Kwa mara ya pili Mnyika aligombea ubunge katika jimbo la Ubungo mwaka 2010 ambapo na akafanikiwa kuingia bungeni kwa mara ya kwanza na kisha akarudi tena mwaka 2015-2020 kwa kupitia jimbo la Kibamba.

Mnyika hakusoma shahada ya sheria (LLB) kama inavyodaiwa na badala yake kwa kipindi hiko alikuwa akisoma shahada ya Usimamizi wa biashara (Masomo ya jioni)

Picha iliyotumika kwenye taarifa hiyo ni kweli ilikuwa ni ya mwaka 2010 katika kampeni za ubunge jimbo la Ubungo eneo la Mabibo ambapo John Mnyika alikuwa mgombea kupitia CHADEMA.
Back
Top Bottom