John Malecela alithubutu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Malecela alithubutu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Dec 1, 2011.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mzee Malecela kipindi akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais alithubutu kutuletea serikali ta Tanganyika akishirikiana na wabunge 55 miongoni mwao Njelu Kasaka na Philip Marmo. Isingekuwa kuingiliwa kati na Mwalimu Nyerere, Malecela angeweza!
   
 2. Pathfinder

  Pathfinder Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 15
  Alikuwa anataka Uraisi tu, hakuwa na lolote....
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka sana jopo lile machachari na kama unafikiri wamelala basi usijilaumu vidonda miguu yote!!! Usimsahau naye mpiganaji wa kimtindo, Mch Mtikila.

   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  kama kweli ilikuwa ni ajenda yake mbona baada ya mwalimu kuingilia kati amekaa kimya hadi leo,?? mpiganaji kamili angetoka ccm na kuanzisha chama au kujiunga na chama chenye sera ya serikali tatu, ila alipowaza uwazi mkuu na umakamu wa raisi na mafao baada ya kustaafu akanywea!!
   
 5. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  lakini pamoja na kutaka urais si angeturudishia Tanganyika yetu?
   
 6. D

  DONALD MGANGA Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Tangayika ipo na itaendelea kuwepo na hivi karibuni itakuwa na miaka 50. Hiyo si Tanzania bara ila ni Tangayika - so hakuna mtu yoyote anaweza kuileta sasa hivi sababu ipo! Tukitaka kujua haipo basi tuangalie jinsi vongozi watakavyo ingia uwanja wa Taifa siku hiyo. PM akiingia kama mtu wa pili kutoka mwisho basi Tangayika Ipo akiingia mtu wa tatu toka mwisho na kuendelea basi tutakuwa tunasherehekea nchi ambayo haipo!
   
 7. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kiprotokali, Pinda yuko chini ya Sharif Hamad!
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Fafanua mkuu au umechanganya mambo.
   
 9. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu, Tanganyika kama 'piece of land' ipo; bali Tanganyika kama 'state' haipo!
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Pia alikuwa na hawara (sasa mke) mwenye kutambua haki na ukweli!

  Zanzibar ipo, Tanganyika iko wapi?
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Pia alikuwa na hawara (sasa mke) mwenye kutambua haki na ukweli!

  Zanzibar ipo, Tanganyika iko wapi?
   
 12. y

  yaya JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, samahani kwa kukuambia kwamba hapo umechemsha. Viongozi wakuu wa nchi ki-protokali ni Rais wa JMTZ, Makamu wa Rais, na baada ya hapo anafuata Waziri Mkuu. Zile za kuwaingiza Rais wa Zanzibar na makamu wake ni fake protocol yenye lengo la kutowaudhi wazenji. Ndiyo maana hata ktk baraza la mawaziri Rais wa Zanzibar ni mjumbe (waziri asiye na wizara maalum). Makamu wote wawili wa Mhe. Rais wa Zanzibar au Waziri kiongozi wote hao hawamo katika baraza la mawaziri, ambalo ndicho kikao kikuu kuliko vyote cha kumshauri Mhe. Rais juu ya mambo yote yanayohusu utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba (ang. ibara ya 54 ya Katiba ya JMTZ).
   
 13. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu! Yawezekana uko sahihi kinadharia lakini uko mbali kabisa na hali halisi. Tukio la kwanza kuwakutanisha viongozi wote wa juu kitaifa ilikuwa ni msiba wa ajali ya meli kule Zanzibar. Itifaki iliyozingatiwa ilikuwa hivi
  1. Rais wa Muungano
  2. Makamu wa rais (muungano)
  3. Rais wa Zanzibar
  4. Makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar
  5. Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar
  6. Waziri mkuu (muungano)

  Tukio linalofuatia wiki ijayo ni sherehe za uhuru, utajiridhisha na hiki nilichokiona Zanzibar. Lakini naungana na wewe kuwa protokali sio mamlaka ndio maana rais znz anakuwa mjumbe tu asiye na wizara maalum katika baraza la mawaziri, lakini anakaa kando ya rais wa muungano. Utakubaliana nami kuwa aliye juu kiprotokali ana ushawishi zaidi kwa mkuu?
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuna uwezekano wale wabunge wa zamani wana G-55 leo hii wakaonekana wamezeeka kinamna fulani hivi ila naweza nikakuhakikishia kwamba yale mawazo waliokua wakiyasimamia ndio kwaaanza yanachipuka miongoni mwa jamii yetu. Time will tell on Tanganyika rejuvination for once!
   
 15. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #15
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  John Cigwiyemisi Malechela ni Mtanganyika halisi!
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280

  kweli alithubutu!
   
 17. I

  Idodi Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  New Tanganyika is coming soon. It might be in the next general erection. It's our time kuthubutu.
   
 18. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  "General election"
   
 19. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,076
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Sahihisha ndugu.
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Endapo katiba italazimishwa kwa ajiri tu ya kufanikisha Project Membe basi kindumbwendumbwe cha TANGANYIKA kurudi kwa kasi na nguvu kubwa ajabu nchini. Mar that point.
   
Loading...