Mkuu, samahani kwa kukuambia kwamba hapo umechemsha. Viongozi wakuu wa nchi ki-protokali ni Rais wa JMTZ, Makamu wa Rais, na baada ya hapo anafuata Waziri Mkuu. Zile za kuwaingiza Rais wa Zanzibar na makamu wake ni fake protocol yenye lengo la kutowaudhi wazenji. Ndiyo maana hata ktk baraza la mawaziri Rais wa Zanzibar ni mjumbe (waziri asiye na wizara maalum). Makamu wote wawili wa Mhe. Rais wa Zanzibar au Waziri kiongozi wote hao hawamo katika baraza la mawaziri, ambalo ndicho kikao kikuu kuliko vyote cha kumshauri Mhe. Rais juu ya mambo yote yanayohusu utekelezaji wa madaraka yake kwa mujibu wa Katiba (ang. ibara ya 54 ya Katiba ya JMTZ).