John Heche: Nitapambana hadi kieleweke Nyamongo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche (CHADEMA) amesema atashikamana na wananchi wa jimbo lake kudai haki za wananchi kwa serikali na kwa mwekezaji katika eneo la Nyamongo kuwalipa fidia wananchi waliotoa maeneo yao kwa mwekezaji.

Heche ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Hot Mix kinachorushwa na kituo cha EATV kuhusu maendeleo ya jimbo lake na jinsi yeye kama Mbunge alivyojipanga.

''Wananchi wa Nyamongo wameteseka vya kutosha na mwekezaji amebakiza miaka 6, mimi nitaongoza jitihada za kuhakikisha wananchi wanalipwa fidia za maeneo waliyotoa kwa mwekezaji wa mgodi wa Nyamongo''-Amesema Heche.

Mbunge huyo ameongeza kuwa katika Mkoa wa Mara Mbuga kubwa ya Serengeti, hawanufaiki nayo kwa namna yoyote kwa sababu kodi zinazopatikana kwenye mahoteli na viingilio vya mbuga hiyo hazibaki katika halmashauri yoyote ya mkoa wa Mara na badala yake zinapelekwa Arusha.

Ameiomba serikali kuangalia upya namna ambavyo wananchi wanaozungukwa na rasilimali watanufaika na rasilimali zao kabla ya kupelekwa maeneo mengine.

"Kuna kipindi hesabu zimeonesha kuwa mgodi huo umeingiza turnover ya bilioni 500 lakini zilizobaki ni bilioni 1 pekee" Amesema Heche.

Aidha mbunge huyo amemkumbusha Rais Dkt. John Magufuli kukumbuka ahadi yake ya kuwatengea wananchi maeneo yao ya kuchimba madini na si kuwaachia wawekezaji wakubwa na kuwaacha wananchi wakiitwa wachimbaji haramu.
 
Mbunge anautumia muda mwingi akiwa mjini mwanza, angangane aonekane bungeni wananchi labda watamwonea huruma
 
Back
Top Bottom