John Heche mwenyekiti mpya BAVICHA taifa

Hata mimi nimemuona nafikiri kuna mwenzake naye anajiandaa yeye demokrasia ya Chadema ni lazima ashinde anayemtaka.

we subiri tu utaona ila nimemiss sana mtaalam wa siasa ya TZ? WABEROYA upo wapi?

Hongera Heche ila tahadhari ni kuwa hapendwi mtu hapa. Kesho ukileta za kigamba utakiona cha mtemakuni.
 
Ingetosha tu kusema una imani na Heche, haya mengine ya CCM kufanya juu chini ili Heche asisinde as if wagombea wengine wa Uenyekiti walikuwa mamluki wa CCM ni hoja ya hovyo kabisa.

By the way wamuogope kwa nini hasa?binafsi naamini pia kuwa Heche kwa kutojua atainufaisha sana CCM Tarime 2015, wait and see!!
Wewe Butola hujui kilichokuwa kinafanyika baada ya siku utaelewa zaidi ndio maana mimi nawapongeza sana wazee kwa kuliona hilo hata Chenge alipogombea Uspika watu hawakujua nia yake lakini baada ya siku kupita wakaanza kuunganisha dot.
 
Hongera sana mkuu,

Sikujui hata kwa sura, sijui ilikuwa na title gani lakini ujasiri wako unanipa kila sababu ya kuamini utakuwa mwiba kwa magamba na wale wanafiki ambao tumbo linawaongoza.

Tuendeleze mapambano.

Hongera bro, futa hisia mbaya za watu kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa manufaa ya chama bila uoga
 
we subiri tu utaona ila nimemiss sana mtaalam wa siasa ya TZ? WABEROYA upo wapi?

Hongera Heche ila tahadhari ni kuwa hapendwi mtu hapa. Kesho ukileta za kigamba utakiona cha mtemakuni.
Umejuaje?
 
i know that man heche from st.Augustne university wa ukweli mbya.chadema nmewakubali kumchagua Heche awa bavicha...congrts mbowe,slaa n al wajumbe
 
Wanao leta na kuhubiri udini, ukanda na ukabila wanafahamika kuwa ni kina nani kutoka mlango wa chama gani. Ameshachaguliwa mwenyekita kwa asilimia 53 hiyo imaana kuwa uchaguzi ulikuwa wa mnyukano. Maneno mengine yasiyokuwa na tija yanatoka wapi?
 
Wagombea Chadema chini ya ulinzi
Saturday, 28 May 2011 21:26
NI KUDHIBITI RUSHWA, MMOJA AENGULIWA KATIKA UCHAGUZI
Godfrey Nyang’oro – mwananchi

UCHAGUZI wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana ulitawaliwa na vituko vilivyoambatana na wagombea wa nafasi ya mwenyekiti, kuwekwa chini ya ulinzi mkali, ili kuwadhibiti wasitoe rushwa kwa wapiga kura. Vituko hivyo vilitokea katiKa mkutano huo wa uchaguzi ulioanza saa 6:00 mchana, katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam na kuendelea hadi usiku.

Katika uchaguzi huo, wagombea tisa wa nafasi ya mwenyekiti, walitolewa nje ya ukumbi wa mkutano na kuwekwa chini ya ulinzi wa mkali wa mabaunsa wawili.Kitendo hicho kilifanyika wakati wagombea hao, wakisubiri kuitwa kwa mahojiano yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wa chama.

Chini ya ulinzi huo, wagombea hawakuruhusiwa kwenda mahali na hata pale walipoitwa kwa mahojiano, walisindikizwa hadi mlangoni.

hii bongo ni balaa kwa rushwa, ina maana wasingewekewa ulinzi??
 
Mbona illikuwa inatarajiwa hii! Kambi ya wenye kampuni wakina Mbowe inazidi kujiimarisha na Kambi ya wakuja wakina Zitto inazidi kudhoofishwa. HABIB na CHADEMA wapi na wapi! Au ulikuwa huamini kuwa chadema ni chama cha watu fulani? Haya umejionea mwenyee hila zao!
 
Angetuchambulia hatma ya CDM baada ya huu uchaguzi.
Hadi sasa hujui atasema nini sisi wengine tuliojifunza mambo ya forecastng na predictions za mawazo ya watu tunajua kuna mtu wao ambaye hakuvuka hata bahari ya shamu ila watu wao wengine walivuka kama Musa lakini Mungu akawaambia kamwe hawataingia kaanani usiniulize zaidi.
 
Mbona illikuwa inatarajiwa hii! Kambi ya wenye kampuni wakina Mbowe inazidi kujiimarisha na Kambi ya wakuja wakina Zitto inazidi kudhoofishwa. HABIB na CHADEMA wapi na wapi! Au ulikuwa huamini kuwa chadema ni chama cha watu fulani? Haya umejionea mwenyee hila zao!
Chadema haiendeshwi kwa hisia zenu za kidini wala haiogopi kuchukua hatua eti itaonekana ni ya dini fulani wamefanya kweli ili mzidi kusema.
 
Mie sina tatizo kabisa na aliyechaguliwa kama taratibu zimefuatwa.
Ni kweli kuwa CDM walienda kuchukua taarifa za mtu kutoka vodacom MPESA? kama ni hivyo, basi huku ni kuingilia privacy ya mtu na sina hakika kama wanaruhusiwa kufanya hivyo. Privacy inakoma kuwa privacy kama kuna public interests na kazi hiyo huhitaji kibali maalum. Wao walipewa kibali hicho na nani?
 
Hadi sasa hujui atasema nini sisi wengine tuliojifunza mambo ya forecastng na predictions za mawazo ya watu tunajua kuna mtu wao ambaye hakuvuka hata bahari ya shamu ila watu wao wengine walivuka kama Musa lakini Mungu akawaambia kamwe hawataingia kaanani usiniulize zaidi.

siulizi tena, nimeelewa kaka.
 
Back
Top Bottom