Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Wakuu!
Makamu Mwenyekiti Bara John Heche, leo tarehe 23 Aprili 2025 anazungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Makao Makuu ya Chama kuanzia saa saba mchana, waandishi wote wa habari mnakaribishwa.
"Jambo la kwanza, tunawaarika Watanzania wote kokote walipo kesho (Aprili 24) Mahakamani waje kusikiliza kesi ya kiongozi wetu Tundu Lissu. Tunawaomba Jeshi la Polisi na Vyombo vya Dola Tanzania wasifanye fujo kwa mtu yeyote, kwa sababu makusudi yetu ya kuja kusikiliza kesi ya kiongozi wetu ni ya amani."
"Kesi hii iko kwenye Mahakama ya wazi, na Sheria zetu kifungu namba 186 zinaeleza kuwa kesi inapokuwa kwenye Mahakama ya wazi ni kwa ajili ya umma, na umma uisikilize. Hii ni kesi kubwa, yenye maslahi ya umma, na ni kesi ambayo hukumu yake ni kunyongwa hadi kufa. Kwa hiyo, hatutaki ifanyike gizani."
"Tunahitaji hii Kesi iwe wazi kwa kila mtu, Vyombo vyetu vya dola vikae pembeni na tunaiomba Mahakama itoe Spika nje Watanzania wapate nafasi ya kusikiliza watakao kosa nafasi (ndani) kinachoendelea ndani ya Mahakama kwasababu Lissu ni kiongozi mkubwa wa Chama cha Upinzani na huwezi kum-try kama una-try tu mtu ambaye amefanya Kesi ya mwizi wa Kuku"
"Nimemsikia Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anaongea anapiga kifua, nimemsikia RPC Murilo anaongea anapiga kifua, Mahakama siyo sehemu yao, hawawezi kuipangia Mahakama nini cha kufanya"
"Haiwezekani nchi yenye Uhuru miaka 63, leo viongozi weusi wenzetu wamkamate mtu wamuwekee kesi ya uongo, kesi yakijinga kabisa (ya treason) kesi ya Kisiasa ambayo wamemuwekea Uhaini wa Kisiasa kujaribu kumnyamazisha kwa misimamo yake ya Kisiasa alafu wazuie hata wanaompenda kuja kumsikiliza"
"Pia tunaitaka Serikali, na tunamtaka Rais Samia kwasababu hii Kesi ni yake, aiondoe hii Kesi Mahakamani wamfutie Lissu hii Kesi ya Uhaini kwasababu ni ya uongo, Lissu sio Muhaini, huwezi kufanya Uhaini kwa Raia ambaye hajawahi kuwa Mwanajeshi, hana kikundi chochote cha Kijeshi anachokiongoza, hawawezi kuithibitisha popote, mwisho wa siku itoakuwa kama Kesi ya Mbowe"
"Ni ajabu kwamba chini ya utawala wa Rais Samia kwa miaka minne ya kwake amejaribu kuwafungulia Viongozi wa Chama hiki kesi mbaya, alijaribu kumfungulia kesi ya ugaidi Mwenyekiti Mbowe ambaye hukumu yake ni kunyongwa mpaka kufa, amejaribu tena kumfungulia Lissu kesi ya uhaini ambayo hukumu yake vilevile ni kunyongwa mpaka kufa"
"Hii kesi iondolewe Mahakamani, Lissu arudi mtaani tuendelee na shughuli zetu kama kawaida"
"Tunaunga mkono tamko la Viongozi wa Dini walilotoa wakati wa Pasaka, tunaunga mkono tamko la Shura ya Maimamu walilolitoa wakati wa Eid wote wakiunga mkono msimamo kama wetu wakisema mabadiliko yanahitajika katika nchi hii ili uchaguzi uwe huru na haki"