Licha ya kupewa kibali cha kufanyia mikutano ya hadhara kwa sharti la kulinda amani, lakini Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ameonekana kushindwa kutumia uhuru aliopewa na sasa ameanza kuamuru vijana wake kuanza kuwapiga wananchi wanaokwenda kuwasikiliza ajenda zao mfu za No Reforms No Election.
Kwanza hali ya hatari ya ilianza kuonekana kwenye mkutano uliofanyika Singida, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche aliwatishia wananchi waliokua na mawazo kinzani kuhusu Hoja yao ya No Reforms No Election na Heche alitamka kauli ambayo ingeweza kuleta maafa makubwa mno kama Jeshi la Polisi lisingekuwepo maeneo ya karibu pale.
Heche alitamka maneno yafutayo "Nyie vijana hapo mnajifanya mnapinga No Reforms No Election, nitawatuma vijana wetu wawafinye hadi mpotee"
Kauli yake hii ilizua taharuki kubwa kwenye mkutano wake wa Singida ambao kwa asilimia kubwa wananchi walikua hawataki ajenda ya No Reforms No Election mpaka pale Polisi walipoingilia kati kunusuru zahma kutokea.
Lakini Chizi huwa hasahau jalala lake, leo tena akiwa mkoani Tabora John Heche ameamuru vijana wake, kuwapiga wananchi waliokwenda kusikiliza hoja zisizo na uhalisia za kuzuia Uchaguzi Mkuu, akaagiza vijana wake kuwarushia mawe wananchi, ambapo mpaka muda huu kuna wananchi zaidi 25 wamejeruhiwa kwa sababu ya kupokea kichapo kwa sababu ya amri ya John Heche.
Umefika muda John Heche aseme wao kama CHADEMA hawawataki Watanzania waende kusikiliza hoja zao zilizokufa, ili waepukane na vichapo kwa sababu ya amri anazozitoa maana kama ni hivyo sasa kila anayekwenda kwenye huo mkutano hana uhakika kama atarudi na Ngeu au kupata ulemavu.