John Cheyo na BoT

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
297

Nakumbuka kuwa ilisemekana Mh. John Cheyo alikatiwa kitu kidogo na akina James Rugemalila wa IPTL akakaa kimya kuhusu ule mradi haramu wa umeme wa IPTL, wakati huo akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya Mahesabu bungeni. Hivi kwenye hizi pilika pilika za BoT hayumo kabisa maana naona amekuwa kimya kwa muda sasa.

Bariadi East legislator John Cheyo (R) exchanges ideas with his Longido counterpart, Lekule Laizer, at the Parliament grounds in Dodoma yesterday. (Photo: Omar Fungo)
 
Una ushahidi hizo pesa alipewa??na lipewa wapi??au ndio udaku wenyewe..
 
Ripoti ya Transparent International iliyoandikwa na Bw. Brian COOKSEY, aliyewahi kufanya kazi REPOA, ndiyo iliyotupa picha ya kirushwa kati ya Mzee Cheyo na IPTL. Nimeiambatanisha ingawa ni ya siku nyingi kidogo. Zaidi pia unaweza kusoma conduct yake kama ilivyoelezewa na Mh. Zitto wa Chadema, kwenye blog yake

Hapa nakuwekea kipande cha yaliyomo ndani ya hiyo riporti, lakini nakushuri uisome kama hukuwahi kuisoma..

Attachments

  • IPTL-TI-Report.doc
    87 KB · Views: 210
Tukianza uchunguzi tanzania naona tutakamata wengi, ndio maana nafikiri kizazi kilichopo kitaondoka bila kufanyi uchunguzi wa mambo mengi sikuwai kujua hili la Cheyo.

Hivi Cheyo aliingizwa na Chenge?
 
Tukianza uchunguzi tanzania naona tutakamata wengi, ndio maana nafikiri kizazi kilichopo kitaondoka bila kufanyi uchunguzi wa mambo mengi sikuwai kujua hili la Cheyo.

Hivi Cheyo aliingizwa na Chenge?

Mkuu Kakindo,
Cheyo labda alipata moja kwa moja toka kwa Rugemalila, maana ni mhongaji wa kupindukia. Alihonga hata maprofesa wa UDSM wakampa degree. Kwa hiyo ingawa Chenge na Cheyo ni damu damu, Rugemalila alikuwa anammudu Cheyo labda baada ya intro fupi tu. Kipindi hiki Cheyo alikuwa hoi bin taabani kipesa, hata na nyumba yake ilikuwa imewekwa rehani.

Ila kwa ambaye hakuisoma hii ripoti ya TI, ni vema kuisoma. Itakupa picha kamili ya kuwa ni nani walikuwa mafisadi waliobobea tokea enzi ya Mkapa, i.e. akina Chenge, Yona, Cheyo n.k., halafu makinda walioambukizwa ndio hao akina Hosea, Rutabanzibwa, n.k. waliokuja kuchachamaa mwishoni. Nafikiri EPA kwa vyovyote itakuwa inamhusu pia Cheyo. Tusubiri data zitapatikana tu.
 
Bw. Mapesa a.k.a Cheyo alionekana kwenye Nipashe ya leo akiuchapa usingizi bungeni.

Baada ya kukoswa koswa kuuziwa nyumba yake Masaki kwa sababu ya deni, ameamua kuwa mtfutaji hela.
 
Muhurumieni bwana mapesa, kwa sasa amechoka kisiasa na ccm si mchezo wamemrusharusha naye akaona akae kimya kuepusha shari,ila msisahau njaa si mchezo
 
Muhurumieni bwana mapesa, kwa sasa amechoka kisiasa na ccm si mchezo wamemrusharusha naye akaona akae kimya kuepusha shari,ila msisahau njaa si mchezo

Mkuu Isaya,
Wachovu kama kama Cheyo hawatakiwi wabakie upinzani na kuendekeza ufisadi. Ni vema akajirudia zake CCM kunakoshabikia matapishi yoyote yatokayo upinzani na kuwazawadia vibarua. Ukiwa upinzani unatakiwa uwe mwaadilifu na wenye nguvu ya kuchapa kazi.
 
Huyu ni kada wa CCM na ndo maana wanamtumia sana wakihitaji wapinzani, hilo sio la kushangaza kwani hawezi hata kuisema serikali hata kidogo hata kama imekosea
 
Muhurumieni bwana mapesa, kwa sasa amechoka kisiasa na ccm si mchezo wamemrusharusha naye akaona akae kimya kuepusha shari,ila msisahau njaa si mchezo

Hawa mafisadi hawana njaa, wangekuwa na njaa wasingeiba kwa kiasi hiki. Wana tamaa inayopita viwango hawatosheki kwa chochote kile.
 
Hawa mafisadi hawana njaa, wangekuwa na njaa wasingeiba kwa kiasi hiki. Wana tamaa inayopita viwango hawatosheki kwa chochote kile.

Nakumbuka Cheyo aliwahi pia kuiba pesa za ruzuku baada ya kufoji vikao vya chama chake ambavyo vilikuwa havikufanyika. Anaonekana kuwa ni fisadi ndani na nje ya chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…