John Cheyo acharuka, awapasha wabunge wa upinzani kurudi bungeni

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,911
2,891
Aliyekuwa mbunge wa Bariadi, mheshmiwa John Momose Cheyo ameeleza kukerwa na kitendo wanachofanya wabunge wa upinzani cha kuonekana maeneo ya bunge huku wakisaini daftari la mahudhurio na kutohudhuria vikao.

Mheshmiwa Cheyo amedai kuwa wabunge hao hawaitendei haki nchi kwa hicho wanachokifanya na anawaagiza mara moja warudi bungeni kuendelea na mijadala.
 
aliye kua mbunge wa bariadi mheshmiwa john momose cheyo ameeleza kukerwa na kitendo wanachofanya wabunge wa upinzani cha kuonekana maeneo ya bunge huku wakisaini daftari la mahudhurio na kutohudhuria vikao mheshmiwa cheyo amedai kua wabunge hao hawaitendei haki nchi kwa hicho wanacho kifanya na anawaagiza mara moja warudi bungeni kuendelea na mijadala.

Duuuhh, pole sana.
Uandishi wako unaonyesha wewe ni mtu wa aina gani.

Cheo anatakiwa ajipashe mwenyewe. Kama anajua kazi za mbunge na alizifanya vizuri kwa nini wananchi wa jimbo Lake walimbwaga.
 
Bw. Cheyo wewe kama nani katika siasa za nchi hii? Kwani wewe ulipokuwa mbunge mbona hao wananchi unaotaka chadema iwasaidie ulishindwa kuwasaidia matokeo yake wakakunyima ubunge?
 
aliye kua mbunge wa bariadi mheshmiwa john momose cheyo ameeleza kukerwa na kitendo wanachofanya wabunge wa upinzani cha kuonekana maeneo ya bunge huku wakisaini daftari la mahudhurio na kutohudhuria vikao mheshmiwa cheyo amedai kua wabunge hao hawaitendei haki nchi kwa hicho wanacho kifanya na anawaagiza mara moja warudi bungeni kuendelea na mijadala.

Cheyo alishajiishia kama mrema tu. Chama gani hakina hata mbunge mmoja. ili amwambie arudi huko bungeni. lini amekua UKAWA mpaka awape ushuri.
 
Nimemsikia Mwanasiasa msaliti wa upinzani bw.John Cheyo akimpokea mwanachama mpya aliyechanganyikiwa bw.Ole medeye.Katika maongezi yake, Bw.Cheyo amejifanya anajua sana Kazi za mbunge kana kwamba chadema hawazijui.Kama Bw.Cheyo anazijua ilikuwaje alishindwa kuzifanya Na kupelekea wananchi wa Bariadi kumpiga chini Na kumchagua mbunge mwingine? Bw.Cheyo unajulikana Kwa undumila kuwili wako fanya ya chama chako Mzee.
 
UJINGA
aliye kua mbunge wa bariadi mheshmiwa john momose cheyo ameeleza kukerwa na kitendo wanachofanya wabunge wa upinzani cha kuonekana maeneo ya bunge huku wakisaini daftari la mahudhurio na kutohudhuria vikao mheshmiwa cheyo amedai kua wabunge hao hawaitendei haki nchi kwa hicho wanacho kifanya na anawaagiza mara moja warudi bungeni kuendelea na mijadala.
UJINGA WAKE KAMA HUU NDIO ULIOMNYIMA KURA JIMBONI KWAKE
 
hapo kwenye "mwanachama mpya aliyechanganyikiwa" nashukuru salamu zimemfikia vilevile kama zilivyomfikia mhe.zitto kwa kuitwa msaliti
 
aliye kua mbunge wa bariadi mheshmiwa john momose cheyo ameeleza kukerwa na kitendo wanachofanya wabunge wa upinzani cha kuonekana maeneo ya bunge huku wakisaini daftari la mahudhurio na kutohudhuria vikao mheshmiwa cheyo amedai kua wabunge hao hawaitendei haki nchi kwa hicho wanacho kifanya na anawaagiza mara moja warudi bungeni kuendelea na mijadala.
CHEYO ni mkono wa CCM. Hatumshangai kwa hilo. Hata alipokuwa mbunge hakuwahi kuwa pamoja na wapinzani wenzie . Hata kwenye bunge la katiba pia. Lakini mwisho wa siku Cheyo, Shibuda, Saidi Arfi, wakakosa ubunge. Na CHADEMA haijafa. CUF haijafa. NCCR haijafa. Na UKAWA UTADUMU DAIMA.
 
Hivi cheyo bado ni mbunge au alipigwa chini? Kama hakuchaguliwa nampa pole akazane kukijenga chama chake huenda 2020 akarudi mjengoni na wakina medeye kupitia UDP
 
Back
Top Bottom