poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 453
- 175
Boko kama kapteni anatakiwa aoneshe nidhamu zaidi na kuwa mfano kwa wengine. Nimemuangalia katika mechi kadhaa yeye ndiye amekuwa mfano mbaya wa mtu asiye na nidhamu.
Mechi ya jana kati ya timu yake ya azam Fc na Yanga amedhihirisha hilo kwa kupewa kadi nyekundu baada ya kuonywa na kadi ya njano awali kwa mchezo usio wa kiungwana.
Ukifuatilia mchezo wa jana baada ya kuchezewa rafu na Juma Abdul wa Yanga, Boko alionesha kulipiza kwa kumchezea Juma rafu tatu za makusudi kitu ambacho hakikuwa Fair.
Baadae akaingia katika purukushani na Kelvin Yondani kiasi cha kutemeana mate na kurushiana ngumi.
Ni kweli yondani alimtemea mate Boko lakini naye baadae akamtemea mate na kumpiga ngumi.
Tuwe wakweli John Boko kwa muda mrefu nidhamu yake imekuwa si nzuri lakini wengi wamekuwa hawamzingatii. Boko hana tofauti na mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa.
Baadhi ya wachezaji wamekuwa wakilalamika kutukanwa au kusemewa maneno ya hovyo na Boko pale wanapopambana nae. Na hili hata Nyosso amelilalamikia.
Boko alimkita mguu Nyosso kwa makusudi kabisa. Siungi mkono kitendo cha Juma Nyosso lakini anagalia mazingira kabla hajafanya tukio hilo.
John Boko kwa nafasi yake kama mshambuliaji na kapteni wa timu fuatilia kadi alizopewa mpaka sasa.
Boko ni mchezaji mzuri na mwenye kipaji anahitaji kubadilika kuwa mfano wa kuigwa kama kapteni wa timu.
Last edited: