Hayo mambo yalishasemwa semwa sana ila uongozi wa Simba kama kawaida yake, unatia pamba masikioni. Wachezaji wa kigeni wanakuja vizuri, wanang'aa haswa, kisha ghafla wanaanza kuflop (e.g Okrah, Baleke,) mara wengine wa namba moja wanapata majeraha na kulazimika kurudi walikotoka (e.g Fraga na Thadeo Lwanga), kisha mwenye namba yake anarudi kwenye nafasi (Jonas Mkude).
Yaani ni kama huku maofisini, ili uweze kukaa ofisini inakulazimu kubadilisha kiti alichokuwa anakalia mtangulizi wako na wewe uweke chako, vinginevyo utapata taabu sana.