Johari aweka wazi kikwazo kutomtembelea Lulu Jela

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
Msanii nguli wa filamu Tanzania Blandina Chagula alimaarufu kama Johari amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa inayomfanya ashindwe kwenda kumtembelea msanii mwenzake wa filamu Lulu Michael gerezani.




jOHARI%20NA%20lULU.jpg

Johari akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana amesema kuwa toka Elizabeth Michael amefungwa hajawezi kwenda gerezani kumtembelea na kumjulia hali kwa kuwa anahofia kwenda kwake ni kuzidi kumuongezea uchungu na upekwe.

"Kiukweli toka Lulu amefungwa jela sijawahi kwenda kumsalimia, kwa upande wangu naona unapokwenda kutembelea ni sawa na kumuongezea machungu na upekwe zaidi hivyo mimi naona hivyo ndiyo maana nakuwa mzito" alisema Johari

Aidha Johari amedai kuwa kitendo cha Kanumba kufariki na kuonekana Lulu alihusika kwenye kifo hicho ni jambo ambalo liliwaumiza sana kwa kuwa watu hao wote walikuwa karibu na wao lakini anaamini kuwa yote hayo ni mipango ya Mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom